Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Vifo vya vijana hawa miaka 80 na early 90 huko ushuani, Oysterbay

Ofcoz zamani ilikuwa rahis kujuana coz community haikuwa kubwa na obay ilikuwa mitaa ya class fulani iliyojitenga tofauti na sasa hv ambapo imejaa watu wa aina tofauti so kujuana sio rahis coz community ishakuwa kubwa/population imeongezeka na eneo limekua la kibiashara zaidi
Na bar za kutosha , hahahahahahaha
 
Sio mmoja alikuwa anaitwa Ipyana nadhani, tumecheza nao sana basketball kwenye half court ya Mzee Malay(rRIP) na kina Mazula, Warioba, halafu tulikuwa tunaenda kuomba mechi na watoto wa Masaki mwisho kina Mpoki(RIP), Eric Mwenda, daaah, zamani kweli mitaa ile tulikuwa tunajiona tunaishi US, mtu jua kali unavaa ki jumper cha hoodie
Tumeingia sana IST kucheza basketball na wototo wa kizungu
Duh ebana kama ni huyo , yuko wwapi siku hizi, tuliamini kabisa eti kachomwa sindano ili arefuke, aisee, nilikua nikimuona basi I felt sorry for him nilikua na ona baba yake atakua katili sana kuchoma sindano ili arefuke, nikiamini atakua tall kiasi cha kuja tisha watu hahahahahah
 
Kuna kitu ambacho sikielewi , kuna mademu walikua wakubwa sana kwangu mimi niko darasa la tatu wao wengine sekondar au darasa la saba huko ,ila nilikua na wapenda na nina wish eti wawe mademu zangu
Leo ngoja ni wataje my childhood crush ( Mnisamehe jamaa najua wengine nita vunja heshima ni wake za watu na tunaheshimiana kwa sasa )

Judy Temu
Masha Macatta
Goudencia Shigella
Annita Mzena
Anna Mbagga
Jamillah Hemed ( nadhani huy u ndio kwao kulikua na video store )
Tibu Mwandoro
Shaka Kirigini
Kisa Kilindu
Titi (sijui last name Alikua anaka Sea Vie )
Tamika Chikawe
Zuhura Kajembo
Husna Katunda
Erica Msangi
Khadija Faraji ( nisamehe dada ila ndio ujue, yani iki muona Michelle Obama na Singer Deseree namuona Khadija tuu )
Jueliet Ngodoki
Stellah Sebwache
Lucy Mality
Pandwe Kalala
Norah Manyama
Na wengine wengi nime sawahau kuwandika hapa , ila sijui nijiite ni malaya wa rohoni nilikuwa maana wote hao nilikua na wish wawe mademu zangu wakati ni wakubwa kwangu sana tuu.
😂😂😂 we ulikua na pepo la ngono tu toka mdogo wala hakuna kingine apo....
 
Huyu nadhani kipindi hicho alikua kaisha zamia Meli , yule hakulelewa kwa Baba yake so hakuwa mmoja ya circle za wana Obay, mimi nime kuja mjua ukubwani akiwa NYC na kelele zake hahahahhahahaha
🤣🤣🤣 boma liwanza
 
Aisee, umenikumbsha Mhalibwa Grocery, huyo Mtafungwa alikuwa anashinda Mhalibwa muda wote unamkuta pale
Tulikuwa tunakaa jirani na sana kina Ntuyabaliwe, wale madada wawili na mdogo wao, Jackline huyo kalikuwa katoto kadogo, mara nimeshaondoka bongo miaka kadhaa, unakuja kusikia ndio Miss Bongo, mara Mrs Mengi, sio Mchezo..
Kina K-Lynn nilikuwa siwajui ina nadhani Sister wake nilikua namuona kwnye Parties za Mwanguku , kama kawaida yangu na shoboka na mademu wakubwa, nilikua namuona demu mkali kinoma, Siku mmoja mshkaji wangu akaniambia , ebana kuna demu mkali kinoma na anaongea naye ,demu wanapiga naye story kwnye simu, amaniambia yuko na ye coco, basi hata sisi tulikua na gari moja la Ukweli ( Sisemi ni lipi) basi nikaenda kumfuata , ebanakuja mkuta nili pigwa butwa demu mkali kinoma kuja kukuta huyo demu ni K-Lynn , alikua mkali zaidi ya alipo kuwa Miss, Jamaa wazushi wakaanza mtisha ooh hutamuweza huyo demu mkali ata chukuliwa na watu, basi jamaa , tukawa tunamfuata K-Lynn Forodhani shuleni , wakati huo nina gari ya maana (ya baba) , ujiko watoto wote wanatutolea macho ,ila jamaa naye akawa domo zege , akamuogope eti wajanja wata mpiku basi haku endelea tukasikaa Victor Mollel ndio ana mfukuzia , sijui kama ali mpata au viipi , Kidogo ukatokea Msiba kwao , ikabidi kwenda mpa pole, baada ya hapo siku msikia tena , Mara ya mwisho niko Mambo Club, naona demu mkali ila ana nywele fupi ( mtoto anajua zana kupiga viwalo) ana dance , kumcheki kumbe ni K-Lynn , duh nika jisogeza msalimia hapo maana alikau kama Shemeji fulani , ingawa hakutoka na mshkaji , basi mimi week hiyo ndio nikaondoka Bongo, sikujua kinacho endelea Mpaka nakuja sikia Kashinda Miss TZ nika sema wow well deserved mtoto mkali kinoma .
 
😂😂😂 we ulikua na pepo la ngono tu toka mdogo wala hakuna kingine apo....
Aisee, sielewi kwanini aisee ina wezekana ni pepo hahahaha , maana sija wahi kuwa na crush na mademu wa rika langu kabisa, yani hakuna demu ambaye nilisoma naye aliye kuwa my childhood crush hata mmoa ila wote ni walikua wakubwa kwangu yani demu walio hang na Kaka zangu ndio hao nilikua na wazimia, hahahahaha
 
Duh, wewe ,unataja wau hapo nime watambua ni Warioba ,Malocho , kwa malocho sikuwahi kwenda kwnye party ila Miriam alisha wahi fanya party ya vijana yani ya Ki brazamen na masista doo, ilifanyika kwa kina Manyeng'a yani ili combintiona ya watu wawili ilikuwa yani Sophia na Miriam, enzi hizo tunaiga mambo ya Kimarekani ya House Pary the movie kama zile zilizo fanyika kwa kina Eddy Sapi .
Komanya ni wepi yule Waziri ? nakumbuka aliamia mwisho mwisho kabisa huku Oysterbay ya sisi wa Kongwe na sikumbuki kama klikuaga na zile party ,
Mahiga ( balozi) sikujua alikaa Obay, kuna Mahiga kaka yake alikaa Oysterbay Mtaa wa Hill road , Mahga balozi alikaa Obay zamani sana miaka ya late 70.s kabla ya kwenda Canada , sikujua kama alikaa Obay .
Bakilana, sikujua kulikua na Bakilana wengine wa huko Mzinga way ,kunaBakilana wale alio kaa huku kama Kenytatta drive au Kaunda dr na kuna hawa walio kaa Msasani road pembeni ya Oysterbay Primary school ,hao wa Mzinga way siwakumbuki .Mtei ni yupi huyo? nlidhani Obay na kumbuka or najua kila mtu.
Party za Warioba zipi hizo , zile akiwa Waziri mkuu ? nakumbuka nilienda paty kama Mbili au tatu , moja sijui ilikua ni birthday ya JUne ,kitu kama hicho , wakiwa wamehamia hapo kwa JUmba la Waziri mkuu ,nili attend hizo ila hazikua nyingi na huyo friend wako wa Geneva ni nani ni ,Simon ? maana Smon alikuwa anakuwepo kwenye party hizo .
Mengi akiishi Msasani Road hiyo longtime sana aisee, hata niko primary school ,hapo Obay , tukikaa kwnye mbuyu pale akipita na Mercedez ndio wana sema wadau huyo mzee ni tajiri Oysterbay Nzima, kumbe uhalisia ni Tajiri Tanzania nzima .
TZA na toyota stoud dah, wachana karibu wote walikua na hizo pick ups ,sijui waliambizana , ilafika wakati , kila familai wana pickup huko obay, matokeo yake wachache tuu ndio wakaw na magari ya ukweli ya vijana kutanulia coco beach ( enzi hizococo beach Jumapili wana jaa watoto wa kishua tuu na kutanuliana mavazi na magari) naw alio tesa na mabari ya ukweli Merrcedez Audi,BMW na kumbuka ni kina Janguoz , Abebez,Yuyu,Mandaraz, Yule jma wa Masaki , walimuuaga Manzese wakidhani ni jambazi, ( nime msahau kina alikua wa Ki Mix wa kiarabu) na wengine wachache nime wasahau kwa hapa .
Ajabu Motie sikumjua kabisa , wala sikuw ahi muona kwnye party zozote za vijana wala coco beach, Motie nime kuja mjua ( Kumuona kwnye kuparty) baada ya kuanza date huyu Seko , tena niliza kumuona Bar One, nilikua na msikia tuu ila kwnye party scenes nilikua simuoni ,s ijui ilikua tuna pishana vipi mpaka nilikua simjui hata ana fananaje, sikumbuki nani nilikua na anz amuona zaidi ni Mdogo wake or Motie .
Abbad Mwinyi hapo nilikua nadhani nilisha Ondoko Bongo , sikumbuki matanuzi yake ila nakumbuka matanuzi ya Abdul Msomali na Albert pia .
Party za kina Eddy Sapi, zilkua kiboko , tulikua tunajiona tuko America kabisa ,kwa jinsi tulivyo kua tuna jidanganya kwa kuiga umarekani kupitia hizo Movies za House Prty .
Wazee wetu Oyesterbay, walikua wana mkosoa sana Mzee Adam Sapi kwa kuruhusu party hizo kufanyika nyumbani kwake, kuruhusu vijana kufanya party bila usimamizi wa wazee.
Kuna siku ilifanyika party hapo the Green,Osyterbay ( Mabembeani) , watu tumesha jiandaa ana kufika hapo , tunakuka mapolice wamejaa na party ime fungwa, kumbe wazee wa Oysterbay wali gundua sijui mnoko gani aliwatonya , basi wazee waka contact Mzee mmoja alikua sijui na cheo gani cha Police anaitwa Mwaitenda (Marehemu) basi akaamuru police wakaja hapo kuzuia party, watu tumesha pigilia Reebok zetu ( High Tops) enzi hizo ndio balaa tena baba kaleta toka UK , tumesha amua wakomesha mabishoo filani ambao walikua wanajiona wanajua sana kupigilia vitu vya Ukweli, ila wao wamevaa FILA sisi tuna Reebok na jensz na Tshirts za Ukweli toka majuu , ilikua tukiingia lazima ugeuke maana enzi hizo viu vya nje ni vichache sana na mpaka mtu Uletewe toka nje ,lasivyo utavaa yuliita "Dar Combined" , yani kila mtu anacho , sasa ujania ilikua ukiingia sehemu unapiga kitu tofauti , uliwakomesha mabishoo fulani fulani, ( Mnajijua kama mna soma hapa ) basi tukatangaziwa hapo kwamba Party hakuna na wote watawanyike kurudi majumbani ,duh, sijui MaDJ ndio walikua kina Abel Siwale (Marehemu) na organizers walikuona Mmoja wapo Franco Mtui (Marehemu), ikawa tafrani tuu , kilammoja hajui nini kifanyike .
Basi watu tukawa so dissapinted , ila kabla hatujaaza kurudi tukasikia wana sema kwamba Eddy Sapi kaenda muomb baba yake tufanyie party kwao, na baba yake kakubali, acha bOnge la shangwe lifanyike ,wote tuka ahamia huko kwa Sapi ( Ilikua party kama ya pili kufanyika hapo) ,ila huw ana shindwa elewa watu ulikua tunapataje taarifa na kulikua hakuna cellphone?, basi Wababa zetu , waka kasirika sana waka kemea vikali Mzee Sapi kuruhusu hizo party kufanyika hapo , lakini wapi tupa piga shangwe mpaka late night .
Beach parties, hizo zilikua za kishua hapo coco beach, hakuna wahuni, ,sijui nani alikuja wa tonya watoto wa Manzese, ikaja kuwa balaa, beach parties zikaja vamiwa na wahuni toka Manzense ( enzi hizo Manzege ni ina wahuni hata Mbagara wanasubiri na Mbagara enzi hizo hata hatuijui na sijui kama ilikuwa na watuw anaishi huko nadhani ilikua pori ) unakuta usiku ziadi ya hata 500 wahuni wakitembea kwa miguu kuja beach Usiku kwnye beach party na ndiopo zikaja acha kufanyika , bila kusaghau zile Pickniks za kibisho , ezi hizo tuna shobo na totoz za Zanaki na Shaban robert.
Miaka ile tume kula maraha sana ,wengine tulidhani labda kukulia America tungekua na fun zaidi, ila baada ya kwwenda US nakuona teenagers wanavyo enjoy life kinamna yao, nikasema Bongo nilikuwa na enjoy zaidi kushinda hawa wahuku ,maana age ina walimit kwnye mambo mengi sana , Bongo ilukua tunajiachia ka raha zote .
Aisee kweli hakuna jipya chini ya jua[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Viwanja vyangu vyote hivyo.

I was out and about.

Maandazi Road ndiyo mama akikuita ukisikia tu "mtoto wangu mzuri..." unajua hii safari ya maandazi road inafuata hapa.

Unalitafuta Toyota Stout la TZA enzi hizo ulichanganye mafuta.

Haile Selassie ndiyo kuanzia St. Peters mpaka IST na Coco Beach, parties za mabalozi na kwa Warioba kama zote.

Mpaka nyingine siwezi kusema hapa.RIP Baba T for lifting me up in the compound.

Kilima nyege hapo nashuka kwenda kwa Bibi Masaki meeting up with my Geneva cousins to catch up, I make a left tMsasani Road nafikiri hapo, to the Bakilanas, na ubalozi wa Ireland huko, nyumba ya Mzee Bakilana ndiyo ipo mwisho wa Mzinga Way, tunatoka parties za alipokaa Mtei tunahamia kwa paries za Bakilana, tunakwenda kupita kwenye kilimanyege chenyewe. Tunaamua, tuende parties za Mzee Malocho, IST, Coco beach, za kwa Marcel Komanya au za balozi Mahiga? parties za posta au za bandari?

Au tunarudi Msasani Road kwa Ronald Mutie Mengi na kulianzisha Oysterbay Hotel huko na ufirauni wa Abbas Mwinyi?

Leo nimeamua tu kuepuka kikombe hiki, nikitaja mengi sana kuna wasiojulikana watanijua mpaka jina.
[emoji23] mkuu wewe ni Rizi moko bhana usituchoshe
 
Asante sana
Haya ngoja niunogeshe uzi wako na kapicha na matukio

Unaona sasa kujichanganya na mashuwa anakuitia mgahawa fulani
Kwa breakfast meeting,unapiga kapuchino huku mziki wa jazz au rock n roll fulani,sjui Country unaisikia kwa mbali
Syo mnaenda sjui shyshy kitambaa cheupe nk eti unaenda for meeting hapo na mtu mnaongelea biashara
Mikelele sjui singeli bongo fleva
Hata hamsikilizani [emoji1]
Hapo kuna picha junction ya kilimanyege nmemuwekea mwanangu
Kiranga inaonekana hapo kafanya sana vurugu na magari


Ova
20230702_095958.jpg
20230702_102331.jpg
20230702_105715.jpg
20230702_105916.jpg
 
"Ipi Malecela straight from London" 🤣🤣🤣🤣

"Lemutuz super brand with American spirit '

Daha hizi damu za mzee Malecela dah wapumzike kwa amani.
Huyo LemuTuz kaja julikana juzijuzi hatukukua naye kabisa wala tulikua hatumjui , hakuwa miongozi mwa zile circles ,Ippy ndio alikua .
 
Haya ngoja niunogeshe uzi wako na kapicha na matukio

Unaona sasa kujichanganya na mashuwa anakuitia mgahawa fulani
Kwa breakfast meeting,unapiga kapuchino huku mziki wa jazz au rock n roll fulani,sjui Country unaisikia kwa mbali
Syo mnaenda sjui shyshy kitambaa cheupe nk eti unaenda for meeting hapo na mtu mnaongelea biashara
Mikelele sjui singeli bongo fleva
Hata hamsikilizani [emoji1]
Hapo kuna picha junction ya kilimanyege nmemuwekea mwanangu
Kiranga inaonekana hapo kafanya sana vurugu na magari


Ova
View attachment 2676015View attachment 2676017View attachment 2676018View attachment 2676019
Hahahahahaha naona uko kwa restourant za ukweli ,huwezi mkuta wa Obay Kitambaa cheupe wala Coco beach ya sasa , mimi nikitaka privacy huwa naenda Coco, huku ni waswazi tuu hakuna anaye kujua , hukutu mtu yoyote akaja kukusalimia , una kuwa free,hahahahahahaahaa
 
Hahahahahaha naona uko kwa restourant za ukweli ,huwezi mkuta wa Obay Kitambaa cheupe wala Coco beach ya sasa , mimi nikitaka privacy huwa naenda Coco, huku ni waswazi tuu hakuna anaye kujua , hukutu mtu yoyote akaja kukusalimia , una kuwa free,hahahahahahaahaa
Mazungumzo ya faragha
Watu mnakaa mnasikilizana
Syo unakaa sehemu sjui kuna mtu
Anacheza juu ya meza singeli
Yaani vurugu

Ova
 
Back
Top Bottom