Vifo vya watu maarufu Iringa vinastusha sana!!

Vifo vya watu maarufu Iringa vinastusha sana!!

20200509_202325.jpg

Nimefurahi kusikia mtu maarufu wa enzi hizo bado Makossa yupo.
 
Kwa takribani siku kumi zilizopita vimetokea mfululizo vifo kadhaa vya watu maarufu hapa Iringa hadi kuzusha maswali mengi sana.

Inawezekana Mungu ameamua kuchukua watu maarufu wanaofahamika hapa Iringa ili kuleta watu wengine maarufu wa kizazi hiki. Lakini inafikirisha sana!!

Sasa unapotuambia kuwa Watu maarufu kadhaa kutoka Mkoani Iringa wamekufa je, umeambiwa wana JF ni Wana Iringa hivyo tunawajua Wote?
 
Kuna taifa fulani la kiimla hapa Afrika mashariki limeamua kuficha vifo vya Corona na wananchi wake wakaamua kukaa kimya kama mazuzu ila nawahakikishia gharama yake ni kubwa
Zuzu wewe chizi we, hao wanaotangaza wameepuka au kupunguza corona? Nini faida ya kutangaza?
Jambo muhimu ni kuelimisha watu wajue adui yupo na wachukue tahadhari kwa kufuata kanuni zlizopo.
Unafurahi kusikia wamekufa wengi au wachache?
 
Kwa watu wa Iringa sawa lakin si kwa kila mtu. Kwa mfano mtoto anayebakwa anapofichwa uso wake siyo kwamba kwa wale walioshuhudia au ndugu zake hawamjui.
Mtu kashakufa unaogopa kumtaja kivipi? Mbona kwenye radio kuna matangazo ya vifo? Babu njenje jana amefariki wamemtaja hadi jina
 
Nmesoma. Chakukufikirisha n nn hapo hao watu maarufu waliokufa wamefika hata kumi. Hv hujawahi kusikia familia moja wamekufa hata watu watano mbona haiwi ishu sana.
Haiwi ishu wakati hadi wanasiasa na media zote zinahamia huko! Kumbuka yule binti aliyefiwa na familia yake waliokuwa wakimfata siku ya mahafali
 
Usibishane na uhalisia wa maisha. Wale watu zaidi ya 100 waliokufa pale Morogoro kwa ajali ya moto unadhani ndani mwao angekuwepo na Paul Makonda unadhani habari ile ingeandikwa kama vile ilivyokuwa imeandikwa.

Kwa mfano si kawaida Polisi kufa kwa kufuatana hapa Iringa tena wote wanaofahamika kwa vifo vinavyofanana. Sasa sisi wana Iringa kushangaa unatushangaa nini?
Kawaida kwako wewe wanakufaga kina nani mfululizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo tumepoke habari za Kifo cha mmojawapo wa watu maarufu sana Iringa Mzee Mwasongwe. Mungu awape faraja wafiwa wote.

1592423611551.png

Pichani ni Marehemu Mzee Mwasongwe akiwa na Mkewe enzi za Uhai wake.
 
Back
Top Bottom