Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Makusanyo ya DPP hatujaelezwa, Yale yalikua ni ya TRA tu.
==
Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Kaskazini, Nancy Nyenga, aliiambia Nipashe kwamba, kwa kiwanda kitakachozalisha vifungashio hivyo, kitatozwa faini ya Sh. milioni 20 na isiyozidi Sh. bilioni moja au kifungo cha miaka miwili jela au adhabu zote kwa pamoja.
Kwa mujibu wa mtendaji huyo wa NEMC, vifungashio vinavyolengwa ni pamoja na vinavyotumika kufungasha ubuyu, barafu na vyote vya plastiki visivyokuwa na nembo ya TBS.
Akizungumzia marufuku hiyo, alisema vifungashio vyote vya plastiki visivyokuwa na nembo ya TBS, havitaruhusiwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu, yaani leo, kwa kuwa serikali imeshapiga marufuku na kuelekeza vifungashio vinavyoruhusiwa.