Iko hivi
Kwanza hii sio kwa Router zote japo Router zote zina hii feature ila namna ya kuipata inaweza ikawa tofauti na jinsi navyoweza kukuelezea mimi.
Kwasababu kila kampuni lina mfumo wake wa mpangilio.
Maelezo haya yatamfaa zaidi yule ambaye anatumia Router ya Airtel 5G.
Kiufupi ni kwamba.
Wewe ukiwa na Router yako ndio umeshika mpini, wewe ndio mwenye maamuzi ya kuamua nani atumie na nani asitumie.
Sasa kupitia Router unaweza ku control na kuona list ya device zilizo unganishwa na WiFi yako.
Kwa hiyo kuna option ya ku block devices ambazo hutaki zipate access ya internet.
Cha kufanya.
- Log in kupitia IP address ya Router ili upate full control.
- Tafuta sehemu ambayo inaonesha list ya device zinazotumia internet yako.
- Kwenye list kila device itakuja na jina lake, kama ni simu ya Tecno basi kwenye device name itaandikwa Tecno.
- Hapo hapo kuna sehemu wameandika taarifa za hiyo device ambazo ni Mac Address na Ip Address
- Note pembeni hizo Mac Address bila kukosea kisha nenda kwenye option iliyoandikwa Firewall
- Ukifika kwenye Firewall tafuta sehemu iliyoandikwa Rules Traffic.
- Ukibonya hapo utaona kuna option maneno mawili yanaonekana ambayo ni whitelist na blacklist, huku neno blacklist likiwa lipo enabled
- Eneo hilo hilo kwenye hayo maneno ya white list na blacklist kwa juu yake utaona option ya IP Address, Mac Address nk.
- Sasa wewe click hapo kwenye Mac Address kisha utabofya sehemu iliyoandikwa add.
- Ukibofya hiyo sehemu itakuambia weka Mac Address, kwa hiyo uta copy hiyo Mac Address ambayo wewe huitambui kisha utai paste kwenye hilo box.
- Kwa chini yake kuna box lingine ambalo hilo unaweza ukaandika chochote tu halafu uka click confirm
- Baada ya hapo itaonesha iyo Mac address ipo kwenye table ya blacklist.
- Hatua ya mwisho uta click save and rule. Hapo ndio unakuwa umeua mchongo
Mtu ambaye amewekwa kwenye hilo jedwali ata connect WiFi lakini hatoweza kupata access ya internet. Yani itakuwa kama mtu aliyewasha WiFi ambayo haina laini so hata uki connect haitafanya kitu.
Kesho nitakuja na clip ili kuweka vitu sawa kama kuna sehemu sijaeleweka.