Broadband ni internet ya staili ipi mkuu
Ipo makundi mengi mengi mkuu Kama vile
-DSL (Digital subscriber line) ambayo hii unatumia zile waya za shaba kusambaza internet, mfano mzuri ni internet ya zamani ya TTCL ambayo ilikuwa inakuja na simu za mezani, na miundombinu yake ni Kama tu ile ya simu za mezani, speed yake kwa sasa imepitwa na wakati.
-Fiber, hii inakuwa ni waya zinasambazwa Kama vile umeme unavyopita, Sasa hivi mijini zipo na Bei zake ni nafuu, unaletewa waya nyumbani unachomeka kwenye router na kusuply internet nyumba Nzima, kwa vifaa Kama simu inatumia wifi na computer unaweza chomeka kwenye Ethernet ama wifi. Hii inakuwa na speed kubwa Sana na pia latency yake ni Ndogo Kama 2ms kwa hapa Tanzania, Halotel pia anayo kaitandaza Nchi Nzima ila anaitumia tu kwenye Mambo yake sidhani Kama ameanza kuipeleka waya majumbani.
-Satelite internet, hii inatumia dishi Kama la Azam vile lakini lenyewe linapokea na kutuma data na kukupa uwezo wa internet. Weakness yake kubwa ni latency sababu ukituma kitu mpaka kiende angani huko kisha ndio kipelekwa mahala husika ila speed ipo ya kutosha,
Wireless, hii unakuta eneo Kama mtaa mtu anafunga router kubwa na kusambaza internet mtaa mzima, mjini pia zipo Kama Maisha broadband, Raha spot etc hizi pia ni za kisasa na Nchi Kama Kenya wanazo nyingi kwa Bei rahisi