Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?

Vigezo gani anavitumia DC wa wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko kuvamia kumbi za starehe na nyumba za wageni kukamata watu anaodai ni makahaba?

Acha tuhamie zetu tabata na temeke huko ubungo usalama ni mdogo sana.

Acha tusubiri afike uwanja wa fisi akute vyumba vyote vina kufuli nje, huwa nawakubali wale wanajua kucheza na code.

Aende manzese pia kila chochoro anawakuta, aisee ataijaza polisi na kufanya askari wetu wapunguze upwiru.

Hawezi tena hawezi kabisa kuikomesha hiyo biashara hata kwa hapohapo sinza tu. Yaani apewe hako kaeneo akomeshe hiyo zaga hawezi.
 
Habari zenu wana jamvi,

Katika pitapita huko mtandaoni nimeona taarifa ya operesheni anayoiendesha Mkuu wa wilaya ya Ubungo,Mh Hassan Bomboko ya kutokomeza biashara ya ukahaba. Takribani miezi miwili amekuwa akiendesha kampeni ya kamata kamata wanawake anaodai ni madada poa na vilevile wanaume wanaodaiwa ni wanunuzi wa makahaba na kama hiyo haitoshi amekuwa akizigungia hadi bar mbalimbali zilizoko Ubungo na Sinza kwa madai ya kwamba zinawahifadhi makahaba.

Swali langu tu ,Je anatumia vigezo gani kuingilia faragha za watu ndani ya nyumba za kulaza wageni kama vile lodge ? Katika video iliyorushwa na Millard Ayo imeonesha akivamia lodge inayofahamika kama PR na kufungua vyumba vyote na kuwatoa watu katika faragha zao kwa madai kuwa ni makahaba na wanunuzi. Je hii ni sawa?

Pia amekuwa akizifungia lodges , je anataka wamiliki wa lodges wawe wanafanya kazi ya polisi kuhoji kazi ya kila mtu anayekwenda kuhitaji kupatiwa chumba cha kulala?

Vp ikiwa mtu amekwenda kupata faragha na mwenza wake katika hizo lodge halafu yeye anavamia na kuwaita watu ni makahaba na wanunuzi wa makahaba?

Kwa hali hii amefungia hadi Bar mbalimbali Sinza kwa kigezo cha kutopuga marufuku makahaba, je hawa wamiliki wanahusika vipi na masuala ya kufahamu kazi za watu?

Haoni kama anawatafutia hasara za kimapato hao wamiliki wa bar na lodges kutokana na kufungia biashara "halali" zinazoingizia Mapato serikali ya Rais Dr Samia Suluhu Hassan.?

Chanzo: Millard AyoTv

View: https://m.youtube.com/watch?v=x4XCJyVLQ7E

Asije tengenezewa mtego wa kupewa ndogo akaingia kwenye mfumo.
 
Jamii zetu bado zinaandamwa na changamoto nyingi sana lakini wao wako katika kupambana na jambo ambalo hata mwenyekiti wa mtaa anaweza kulitekeleza, lkn kwa kuwa hawa Viongozi wetu akili zao ni fupi kama maisha ya funza, na wanataka kufanya kazi za kuonekana ili aliyewateuwa awaone sasa hao waliowakamata watawashtaki kwa sheria ipi? watu umewakuta wako ndani faragha tena gesti unaanzaje kusema kwamba wanajiuza hivi akiitwa mahakamani aje atowe ushahidi ataweza kuiaminisha mahakama kama kweli hawa wanawake walikuwa anajiuza pasipo na ushahidi wowote? Hii nchi ina viongozi takataka sana, Viongozi wengi tulionao katika serikali hawana mawazo ambayo ni productive wengi ni takataka kabisa.
 
Hivi ni kwanini hata asingemtafuta Mwanasheria wa Manispaa ya Ubungo classmate wangu Wakili Msomi Coletha ampe ABC za kisheria kuhusu ukahaba?

Kwanini viongozi wa umma wanajidhalilisha?

Kwanini hata asingepita humu JF akasoma kisa cha RC wa Dar 1985 bwana Joseph Rwegasira na suala la kupambana na ukahaba na usia aliopewa na Nyerere?
 
Hivi ni kwanini hata asingemtafuta Mwanasheria wa Manispaa ya Ubungo classmate wangu Wakili Msomi Coletha ampe ABC za kisheria kuhusu ukahaba?

Kwanini viongozi wa umma wanajidhalilisha?

Kwanini hata asingepita humu JF akasoma kisa cha RC wa Dar 1985 bwana Joseph Rwegasira na suala la kupambana na ukahaba na wosia aliopewa na Nyerere?
Sasa kama hao Viongozi wenyewe wanateuliwa kwa kuangaliana kuwa ulikuwa mtoto wa kiongozi gani pasipo kuzingatia uwezo, unadhani wanaweza kuwa na mawazo ambayo ni productive? Hao ma DC wengi ni baba kantuma hakuna viongozi humo.
 
Kabisa yani, kuna mambo mengi ya msingi ya kushughulikia hivi mkuu wa wilaya unaenda kukagua gesti kweli? hivi amekosa kabisa shughuli nyingine za kufanya ?
Ni wavivu na kupenda sifa aonekane km hivyo kwenye media mama amuone anapiga kazi, si ajifunze kwa DC makini na mchapa kazi NICKSON SIMON
 
Anatafuta sifa za kijinga wakati wilaya ina changamoto kibao. Sasa hiyo inawasaidia nini wananchi wa eneo lake?? Hawa ma DC mizigo, kuna vyeo vilitakiwa kufutwa.
Ametokea Ukerewe DC. Kabla ya hapo alikuwa Katibu Hamasa wa Chipukizi wa UVCCM.

DC huyu aisee!
 
Anatafuta sifa za kijinga wakati wilaya ina changamoto kibao. Sasa hiyo inawasaidia nini wananchi wa eneo lake?? Hawa ma DC mizigo, kuna vyeo vilitakiwa kufutwa.
Hawa wengi waliteuliwa kwa vimemo kulingana na nyadhifa walizokuwa nazo baba, mama, wajomba zao, kwa hali hii ya kuteuwa pasipo kuangalia uwezo wa mtu, bado tutaendelea kuwa nchi ya Ahadi miaka yote.
 
Sasa kama hao Viongozi wenyewe wanateuliwa kwa kuangaliana kuwa ulikuwa mtoto wa kiongozi gani pasipo kuzingatia uwezo, unadhani wanaweza kuwa na mawazo ambayo ni productive? Hao ma DC wengi ni baba kantuma hakuna viongozi humo.
Hata kama aisee. Too low to think!
 
Hawa wengi waliteuliwa kwa vimemo kulingana na nyadhifa walizokuwa nazo baba, mama, wajomba zao, kwa hali hii ya kuteuwa pasipo kuangalia uwezo wa mtu, bado tutaendelea kuwa nchi ya Ahadi miaka yote.
Na ndio tatizo hilo
 
Kabisa yani, kuna mambo mengi ya msingi ya kushughulikia hivi mkuu wa wilaya unaenda kukagua gesti kweli? hivi amekosa kabisa shughuli nyingine za kufanya ?
Viongozi hawana maarifa hawataki wakosolewe wanafanya kazi kwa sifa
 
Back
Top Bottom