Tetesi: Vigogo waliosimamishwa kazi waajiriwa sekta binafsi, waendelea kupokea mishahara ya serikali

Vigogo watano waliosimamishwa kazi kutoka Bohari kuu ya madawa (MSD) pamoja na halmashauri mbili nchini wameula katika sekta binafsi huku wakilipwa mishahara ya kuanzia milioni mbili na nusukwa mwezi (take home). Aidha vigogo hao bado wameendelea kulipwa asilimia hamsini ya mishahara yao serikalini.

Hayo yanajiri huku kigogo mwingine aliyesimamishwa kazi TTCL akitarajiwa kusaini donge nono katika kampuni moja ya uzalishaji hapa nchini. Vigogo hao ambao majina yao yanahifadhiwa, wote kwa pamoja wanaendelea kulipwa nusu ya m ishahara yao ya awali pamoja na stahiki nyingine kama kawaida wakati ambapo tayari wameajiriwa ndani ya sekta binafsi.

Aidha kigogo mwingine wa TRA aliyesimamishwa kazi kwa kudaiwa kuhusika na wizi mkubwa wa mapato ndani ya shirika hilo naye ameula ndani ya kampuni moja kubwa ya madini nchini huku mshahara wake ukikadiriwa kufika milioni kumi na tano kwa mwezi!

Kuna haja ya kuliangalia upya swala hili!!!
Huyo wa TRA anawafundisha tax avoidance and probably how to cover their tracks. Wahasibu walio specialize kwenye masuala ya tax nadhani ndio wanaopata ki pato kikubwa kwa sasa.
 
Mlisema lowassa ana mtandao mkubwa ngoja tuone 2020 yaani hapa tunang'oa miti mizizi mpaka udongo na bado system yote aliyokuwa nayo tunafyeka hamjiulizi kwann mbowe ameanza kukingia kifua majipu na bado
Magufuli akomae nayo. Dau keshapata ubalozi?
 
Wewe utakuwa bawacha maana ndiyo huwa mnaandika uandishi wa namna hii sijui nani kawaroga nyie wanawake wa bawacha.
 
Vigogo watano waliosimamishwa kazi kutoka Bohari kuu ya madawa (MSD) pamoja na halmashauri mbili nchini wameula katika sekta binafsi huku wakilipwa mishahara ya kuanzia milioni mbili na nusukwa mwezi (take home). Aidha vigogo hao bado wameendelea kulipwa asilimia hamsini ya mishahara yao serikalini.

Hayo yanajiri huku kigogo mwingine aliyesimamishwa kazi TTCL akitarajiwa kusaini donge nono katika kampuni moja ya uzalishaji hapa nchini. Vigogo hao ambao majina yao yanahifadhiwa, wote kwa pamoja wanaendelea kulipwa nusu ya m ishahara yao ya awali pamoja na stahiki nyingine kama kawaida wakati ambapo tayari wameajiriwa ndani ya sekta binafsi.

Aidha kigogo mwingine wa TRA aliyesimamishwa kazi kwa kudaiwa kuhusika na wizi mkubwa wa mapato ndani ya shirika hilo naye ameula ndani ya kampuni moja kubwa ya madini nchini huku mshahara wake ukikadiriwa kufika milioni kumi na tano kwa mwezi!

Kuna haja ya kuliangalia upya swala hili!!!
Unadhani ndo watakurudisha? Hatishiwi mtu nyau hapa,kama mmepata nendeni huko huko wala usitegemee kuwa pengine serikali itahangaika kuwarejesha wezi kazini maana wapo wenye vyeti,ujuzi na watiifu wa kazi wengi tu Tanzania hii.
 
Back
Top Bottom