The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katika tukio la kushtua, vijana 132 wenye umri kati ya miaka 18 na 22 kutoka mikoa mbalimbali ya pembezoni mwa Tanzania wamekamatwa huko Mlandizi, Kibaha Vijijini mkoani Pwani, wakiwa wanajihusisha na biashara ya mtandaoni inayodaiwa kuwa ni ya kitapeli.
Biashara hii inadaiwa kufanyika kwa usiri mkubwa chini ya kampuni ya QI Group of Company yenye makao makuu nchini Malaysia.
Tukio hili lilitokea usiku wa kuamkia Februari 15, majira ya saa tatu usiku hadi saa saba, ambapo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Salim Morcase, akiwa na maafisa wa polisi walifanya msako wa ghafla na kuwakuta vijana hao pamoja na viongozi wao katika nyumba tatu tofauti.
Morcase alibainisha kuwa mafanikio ya kukamatwa kwa vijana hao ni kutokana na taarifa za kiintelijensia, ambazo zilionesha kuwa wanajishughulisha na shughuli zinazovunja sheria na zinazotishia usalama.
Aliongeza kuwa baadhi ya viongozi wa mtandao huo wamekamatwa na watafikishwa kwenye mahojiano na uchunguzi zaidi, na kwamba taratibu za kisheria zitachukuliwa.
Baadhi ya vijana waliokamatwa walieleza kuwa walivutiwa na ahadi ya ajira mtandaoni baada ya kushawishiwa na wenzao.
Baadhi ya mikoa wanayotoka vijana hao ni pamoja na Mikoa Mbeya,Songwe, Ruvuma ,Songea, Tabora,Singida ,Kilimanjaro. Katavi,Mtwara , Dodoma . Kigoma , Mwanza, Manyara. na Arusha