Vijana 132 wakamatwa Kibaha wakijihusisha na biashara ya mtandaoni inayodaiwa ni utapeli

Vijana 132 wakamatwa Kibaha wakijihusisha na biashara ya mtandaoni inayodaiwa ni utapeli

Je hiyo biashara ya mtandaoni inayodaiwa ni utapeli inafanyikaje?
Kwa sababu za usalama jinsi biashara hiyo inavyofanyika imebakia kuwa siri hadi hapo uchunguzi zaidi utakapokamilika. Vinginevyo wajanja wataingia msituni na kuanza kututia hasara.
 
Kuna jamaangu mmoja alikuwa ananisihi kila siku niende huko kibaha ila nikimwambia anipe maelezo kidogo kuhusu hiyo ishu lakini ananiambia nifike ofsini nitapata maelezo yote ila baadae nikasanuliwa na mshkaji mwingine kuwa wanajisshughulidha na biashara ya utapeli mitandaoni nilishangaa sanaa
 
Kifupi unaweza kukuta hawana kesi sasa ndo nini hv
Biashara ya mtandao wanajiuza telegram au wanauza bangi Kwa njia ya mtandao ,,n lini police CCM mtajua kueleza dhumuni la kesii na c siasaa km hv🤔
 
Katika tukio la kushtua, vijana 132 wenye umri kati ya miaka 18 na 22 kutoka mikoa mbalimbali ya pembezoni mwa Tanzania wamekamatwa huko Mlandizi, Kibaha Vijijini mkoani Pwani, wakiwa wanajihusisha na biashara ya mtandaoni inayodaiwa kuwa ni ya kitapeli.

Biashara hii inadaiwa kufanyika kwa usiri mkubwa chini ya kampuni ya QI Group of Company yenye makao makuu nchini Malaysia.

Tukio hili lilitokea usiku wa kuamkia Februari 15, majira ya saa tatu usiku hadi saa saba, ambapo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Salim Morcase, akiwa na maafisa wa polisi walifanya msako wa ghafla na kuwakuta vijana hao pamoja na viongozi wao katika nyumba tatu tofauti.

Morcase alibainisha kuwa mafanikio ya kukamatwa kwa vijana hao ni kutokana na taarifa za kiintelijensia, ambazo zilionesha kuwa wanajishughulisha na shughuli zinazovunja sheria na zinazotishia usalama.

Aliongeza kuwa baadhi ya viongozi wa mtandao huo wamekamatwa na watafikishwa kwenye mahojiano na uchunguzi zaidi, na kwamba taratibu za kisheria zitachukuliwa.

Baadhi ya vijana waliokamatwa walieleza kuwa walivutiwa na ahadi ya ajira mtandaoni baada ya kushawishiwa na wenzao.

Baadhi ya mikoa wanayotoka vijana hao ni pamoja na Mikoa Mbeya,Songwe, Ruvuma ,Songea, Tabora,Singida ,Kilimanjaro. Katavi,Mtwara , Dodoma . Kigoma , Mwanza, Manyara. na Arusha

View attachment 3237197
Kwa nini hakuna hata mmoja kutoka mkoa MARA, Je hii ni kwa sababu hawajui kutumia fursa au ni welevu sana wakugundua michezo?
 
wambulu wamekua wahanga wa kutapeliwa kila mwaka na biashara za alinacha ponzi schemes, wamejaa QNET na LBL kama mchwa na siafu. HAWAKOMI
 
Bila huba, Wala Upendeleo, ningewasihi vijana waone hizi fursa zinazofunguliwa na serikali Kila uchao, mfano MUST (Udsm Mbeya campus)wametoa nafasi za mafunzo ya ufundi na ujuzi buuure kwa vijana haswa wa mikoa hiyo ya Karibu na yanaenda mpaka miezi sita, Kuna mikopo ya asilimia kumi (ingawa bado Ina ukiritimba na mwingi licha ya Maboresho) hapo nyuma mashirika mengi yalisomesha vijana ufundi Bure na kwa dar Kuna vyuo vya veta rasmi viliingia ubia nahayo mashirika ikiwemo USAID. Kwanini bado watu wanashawishika kufuata upatu kisa ndugu zao? Na kwa gharama kubwa? Mfano huyo dada anasema alianza na kununua bidhaa za 2.5m .

Pia na serikali ione hali ilivyo mbaya kwa vijana Hawa wadogo wanaokosa fursa za ajira endapo kungekuwa na viwanda, vikubwa ( manufacturing industries) vya kati na vidogo.
Hao ambao tayari wana ujuzi, bado wanahangaika kwa kutekekezea huo ujuzi walionao. Lol

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Taarifa ndefu sana lakini haijataja hata kwa kifupi ni Biashara gani.

Kaole sanaa group
Ni kama Desi au zile Q net (jina sijui kama nimepatia vizuri). Unaalika mtu anaweka bond ya fedha ya kitu na yule naye anamwalika mwenzake yaani ni hizi njia za utapeli.
 
😂😂😂 ndio mimi aisee, mimi ni afisa kipenyo hapo niliingia kama mole ili niujue mfumo vizuri niwalipue, hao polisi wamekuja baada ya mimi kuwaambia waje sasa nshamaliza kazi.
Hovyo kabisa wewe 😂😂😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom