Vijana 149 wahitimu mafunzo ya Mgambo. Je ni maandalizi ya Uchaguzi?

Vijana 149 wahitimu mafunzo ya Mgambo. Je ni maandalizi ya Uchaguzi?

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Vijana waliohitimu mafunzo ya jeshi la Akiba wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wametakiwa kuishi kiapo walichoapa pamoja na kutumia vizuri mafunzo waliyoyapata katika kipindi chote Cha mafunzo ili kuendelea kuwa wazalendo.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Ambrosi Lijualikali wakati akifunga mafunzo hayo katika viwanja vya sabasaba vilivyopo Mji mdogo wa Namanyere.

Awali akitoa taarifa mwakilishi wa Wahitimu wa Mafunzo ya Mgambo, Charles Peter amesema licha ya mafanikio waliyoyapata katika mafunzo hayo wamekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo Ukosefu wa yunifomu hali iliyopelekea kuhitimu mafunzo yao wakiwa hawana sare.

Akijibu changamoto ya Ukosefu wa sare ziliizoelezwa na wahitimu wakati wakisoma risala Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nkasi kutatua changamoto hiyo kwa kutenga bajeti na kuandaa sare za jeshi la akiba zisizopungua 200, ili waweze kuzitumia katika shughuli mbalimbali za kiserikali.

Meja Josephat Mtaka Mwakilishi wa Mshauri wa Mgambo wilaya ya Nkasi ambae ni Mshauri wa Mgambo wilaya ya Sumbawanga mjini na vijijini amesema Mafunzo hayo ya jeshi la akiba yalianza Mwezi April mwaka huu yakianza na vijana 180 na kuhitimishwa leo August 20, 2025 na vijana 149 Wanaume 136 na wanawake 13.



1755766290461.png

​
Source: Clouds TV
​
 
Back
Top Bottom