Vijana 2 wachomwa moto kwa madai ya wizi wa simu Arusha

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Vijana wawili ambao majina yao hayajafahamika wamechomwa moto wao na pikipiki waliyokuwa wakiitumia katika eneo la Shivaz katika kata ya Kaloleni Mkoani Arusha wakidaiwa kuiba simu

Lilia Shayo amesema vijana hao walikuwa wamemuibia mwananchi mmoja simu na wakati wanakimbia walizuiwa na wananchi nakuanza kuwashambulia.


Wiki mbili zilizopita vijana wengine wawili walinusurika kuuawa huku risasi moja ikifyatuliwa hewani baada ya vijana hao kuiba simu jambo lililopelekea wananchi kuichoma moto pikiiki waliyokuwa wanaitumia

Baada ya vijana hao kuchomwa moto walichukuliwa na askari wa jeshi la polisi baada ya wananchi wenye hasira kali kuwachoma moto.
 
Safi sana, bado mawaziri ndani ya serikali. Sheria ipitishwe ya kukamata mawaziri na viongozi wa serikali wezi tuwachome moto ili liwe fundisho kwa wengine.
 
Hivi ni matatizo ya akili au nini yaani kitendea kazi unacho badala kukitumia kwaajili ya kufanya shughuli halali ya bodaboda mtu unajiingiza kwenye uwizi
Huku morogoro tunaita vishandu wakikupora simu wako tayari kufa sitasahau walinipora simu tarehe 29-12-2021 nikiwa nyuma kwenye bajaj kama abiria huwa wanatumia boda kupora simu hadi leo hiyo simu sijaipata
 
Wewe ni Mtaliban? Kwanini usianze wewe kuwashambulia hao wezi wa mabilioni?
 
Mwenye kundi lake anasemaje maana alitangaza hadharani kuwa amewatakasa ni wazuri sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…