Vijana 2 wachomwa moto kwa madai ya wizi wa simu Arusha

Vijana 2 wachomwa moto kwa madai ya wizi wa simu Arusha

Vijana wawili ambao majina yao hayajafahamika wamechomwa moto wao na pikipiki waliyokuwa wakiitumia katika eneo la Shivaz katika kata ya Kaloleni Mkoani Arusha wakidaiwa kuiba simu

Lilia Shayo amesema vijana hao walikuwa wamemuibia mwananchi mmoja simu na wakati wanakimbia walizuiwa na wananchi nakuanza kuwashambulia.


Wiki mbili zilizopita vijana wengine wawili walinusurika kuuawa huku risasi moja ikifyatuliwa hewani baada ya vijana hao kuiba simu jambo lililopelekea wananchi kuichoma moto pikiiki waliyokuwa wanaitumia

Baada ya vijana hao kuchomwa moto walichukuliwa na askari wa jeshi la polisi baada ya wananchi wenye hasira kali kuwachoma moto.
Huo ndio mshahara wa wizi haswaa kama wamedakwa red handed
 
Hivi ni matatizo ya akili au nini yaani kitendea kazi unacho badala kukitumia kwaajili ya kufanya shughuli halali ya bodaboda mtu unajiingiza kwenye uwizi
Hawa mara nyingi huwa wanaomba deiwaka kwa washkaji zao bodaboda halafu wanaenda kuzitumia katika uhalifu
 
Wanataka hela nyingi ya harakaharaka.
Hizo hela zenyewe za harakaharaka wanazozitaka hakuna cha maana watakachofanyia zaidi ya kulewea na starehe ndogondogo tu na Matokeo yake ndo hayo
 
Mwafrika ni mtu wa hovyo sana. Tzama hata viongozi wetu wamekwapua ma bilioni y fedha lakini bado hawaridhiki na ukiwazuia kuingia madarakani wanakutoa roho.

Yaani wana mitaji ila wanakandamiza watoto wa maskini ndio wajiajiri ila wao hapana.

Sasa imagine mtu ana boda boda inayoingiza fedha kila siku lakini anataka za haraka haraka za kukwapua tu.

Juzi Dada yangu kakwapuliwa IPhone yake mchana kweupe saa nane.
Tunasafari ndefu sana
 
Hawa mara nyingi huwa wanaomba deiwaka kwa washkaji zao bodaboda halafu wanaenda kuzitumia katika uhalifu
Hata udeiwaka ukitulia huwezi kosa hela ya kula maana ile mara nyingi haina hesabu ni katika hali ya kugawana riziki tu kwa madereva
 
Wewe ni waziri wa nini hapa nchini maana naona umenijibu kwa hasira mno kwa kuwa umeguswa.
Hiko unachokitafuta, hakito timia kwa viongozi hawa kwa katiba hii, kwa aina yenu ya raia mliopo, si mpaka niwe waziri, ila mtu wa kawaida tu anaona
 
Back
Top Bottom