Vijana 60,000 wanapowania nafasi 1,000 za ajira

Vijana 60,000 wanapowania nafasi 1,000 za ajira

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,557
Nina imani hao niwachache tu waliojitokeza kwani bado huku mitaani tumebaki wengi ambao hatuku apply nafasi hizo za TRA,hii ni hatari!ajira sasa ni kama bomu la nyuklia

Hapa cha kushauriKwanza, serikali kupitia Wizara za kazi,fedha na ofisi ya waziri mkuu kuangalia namna ya kutengeneza ajira kwa vijana kwani kila mwaka idadi mitaani inaongezeka

Zifanyike juhudi za maksudi kutumia mabonde na mashamba makubwa ya chai,tumbaku,mpunga,mahindi,mboga mboga,uvuvi,miti na hata ufugaji kuwaingiza ajira vijana humo kwa serikali kuwasapoti kwa kununua matrekta mengi kujenga kambi kwa maana ya nyumba nyingi jirani na mashamba hayo mikoani, kuwawekea huduma zote muhimu za hospital,shule,mabenki nk,vijana wazalishe mazao yachakatwe serikali ifanye export.

Pili, serikali iwawekee milango wazi na kuondoa ugumu wa kupata hati za kusafiria kwa maana ya bei ya pasi na ulazima wa mtu kuulizwa anaenda nje kufanya nini,wananchi wote wapewe hati za kusafiria na serikali ihimize watu watoke kwenda nchi tofauti duniani kutafuta maisha huko,viwandani,mashambani,mahotelin,madereva,mafundi,migodini,wauguzi,na wengine kutangaza utamaduni,lugha ya kiswahilii nk kama walivyozagaa mataifa ya wenzetu duniani hususan wakenya,Nigerians nk

Yakifanyika haya kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira litapungua

Nawasilisha.
 
Kuna Dr mmoja alinambia hii Nchi utabadilishwa na vijana..
Either kwa amani au kwa fujo sababu hali ikiendelea hivi hivi baada ya miaka mitano tutakua na taifa lenye vijana jobless wengi saana so wataona nini cha kufanya..

BTW na ambao hawajasoma pia wako wengi saana, ukiona umepata nafasi ya kufanya kazi mshukuru Mungu then fanya kazi kwa moyo.

Nla
 
Chini ya mboga party utakuta kila aliyepitia ikulu anahakikisha immediate family members wake wanapata kazi za serikali Kama sio ubunge.
Ukiondoa mzee Mkapa na baba wa Taifa.
Hilo ndio la kwanza yani “kuitana kwenye sinia la pilau”
La pili ni mchongo wa kukwapua hela kulimbikiza kwenye account za nje
 
Pili, serikali iwawekee milango wazi na kuondoa ugumu wa kupata hati za kusafiria kwa maana ya bei ya pasi na ulazima wa mtu kuulizwa anaenda nje kufanya nini,wananchi wote wapewe hati za kusafiria na serikali ihimize watu watoke kwenda nchi tofauti duniani kutafuta maisha
Hapo red, wala hilo sio Tatizo Kuipata mkuu. Ukiwa na docs zote within 2 weeks wanapata labda wapunguze bei kidogo. Ila Tatizo pesa/nauli looh, Tangu niipate yangu kribia inaExpire Sijawahi kuitumia hata hapo Namanga. Nadhani Wangeweka mfumo wa kukopesha pesa(Nauli snd other expenses) kwa ambao wanataka kwenda nje wakiwa na sifa halafu wawe wanakata hela yao taratibu.
Anyway naona serikali haina nia na mipango ya kuinua vijana wa taifa hili....Wacha tuendelee kukaba na kuiba kuku mitaani na kunywa Viroba😢🚶🚶🚶
 
Nina imani hao niwachache tu waliojitokeza kwani bado huku mitaani tumebaki wengi ambao hatuku apply nafasi hizo za TRA,hii ni hatari!ajira sasa ni kama bomu la nyuklia
Hapa cha kushauri

Kwanza,serikali kupitia wizara za kazi,fedha na ofisi ya waziri mkuu kuangalia namna ya kutengeneza ajira kwa vijana kwani kila mwaka idadi mitaani inaongezeka

Zifanyike juhudi za maksudi kutumia mabonde na mashamba makubwa ya chai,tumbaku,mpunga,mahindi,mboga mboga,uvuvi,miti na hata ufugaji kuwaingiza ajira vijana humo kwa serikali kuwasapoti kwa kununua matrekta mengi kujenga kambi kwa maana ya nyumba nyingi jirani na mashamba hayo mikoani,kuwawekea huduma zote muhimu za hospital,shule,mabenki nk,vijana wazalishe mazao yachakatwe serikali ifanye export.

Pili, serikali iwawekee milango wazi na kuondoa ugumu wa kupata hati za kusafiria kwa maana ya bei ya pasi na ulazima wa mtu kuulizwa anaenda nje kufanya nini,wananchi wote wapewe hati za kusafiria na serikali ihimize watu watoke kwenda nchi tofauti duniani kutafuta maisha huko,viwandani,mashambani,mahotelin,madereva,mafundi,migodini,wauguzi,na wengine kutangaza utamaduni,lugha ya kiswahilii nk..kama walivyozagaa mataifa ya wenzetu duniani hususan wakenya,Nigerians nk

Yakifanyika haya kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira litapungua

Nawasilisha.
Hayo yote kamuambia Baba ako. Sio kuliambia lizimwi ambalo lipo kila sehemu"Serikali".
 
Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.

1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.

2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.

3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele

4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao.

Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.

5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue.

Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.

6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa

Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana ccm imeshindwa nini.
 
Hata waliobahatika kufanya mtihani wanalalamika awakutendewa haki.
Waliingizwa chumba cha mtihani kwa usimamizi wa police wakaponywa saa wote mtihani ni dakika 40 maswali magumu baada ya dakika 10 wakaambiwa zimebaki daki 10 wakaanza kuguna na kulalamika, wakapigwa biti atakaelalamika atafutiwa mtihani. So azikutimia dakika 40 wakaambiwa simama juu watu wametoka walilalamika wamechoma bure nauli zao toka mikoani.
 
Hata waliobahatika kufanya mtihani wanalalamika awakutendewa haki.
Waliingizwa chumba cha mtihani kwa usimamizi wa police wakaponywa saa wote mtihani ni dakika 40 maswali magumu baada ya dakika 10 wakaambiwa zimebaki daki 10 wakaanza kuguna na kulalamika, wakapigwa biti atakaelalamika atafutiwa mtihani. So azikutimia dakika 40 wakaambiwa simama juu watu wametoka walilalamika wamechoma bure nauli zao toka mikoani.
Wajanja sana wanakusanya kwenye dk 36 ivi inahitaji timing sana
 
Rafiki yangu katoka Mwanza Alhamis iliyopita kwa ajili ya huu usaili juzi akaniambia anaona roho inasita haendi tena kwenye usaili.

Kwahiyo jamaa jana tukaamka saa moja asubuhi tukacheza FIFA mpaka saa saba usiku, nimeamka muda huu ndiyo nakuta haya malalamiko.
 
Chini ya mboga party utakuta kila aliyepitia ikulu anahakikisha immediate family members wake wanapata kazi za serikali Kama sio ubunge.
Ukiondoa mzee Mkapa na baba wa Taifa.

Jina Mkapa ondoa halipaswi kuwa sambamba na Nyerere au umesahau walivyogawana nyumba za serikali?
 
Back
Top Bottom