Nina imani hao niwachache tu waliojitokeza kwani bado huku mitaani tumebaki wengi ambao hatuku apply nafasi hizo za TRA,hii ni hatari!ajira sasa ni kama bomu la nyuklia
Hapa cha kushauriKwanza, serikali kupitia Wizara za kazi,fedha na ofisi ya waziri mkuu kuangalia namna ya kutengeneza ajira kwa vijana kwani kila mwaka idadi mitaani inaongezeka
Zifanyike juhudi za maksudi kutumia mabonde na mashamba makubwa ya chai,tumbaku,mpunga,mahindi,mboga mboga,uvuvi,miti na hata ufugaji kuwaingiza ajira vijana humo kwa serikali kuwasapoti kwa kununua matrekta mengi kujenga kambi kwa maana ya nyumba nyingi jirani na mashamba hayo mikoani, kuwawekea huduma zote muhimu za hospital,shule,mabenki nk,vijana wazalishe mazao yachakatwe serikali ifanye export.
Pili, serikali iwawekee milango wazi na kuondoa ugumu wa kupata hati za kusafiria kwa maana ya bei ya pasi na ulazima wa mtu kuulizwa anaenda nje kufanya nini,wananchi wote wapewe hati za kusafiria na serikali ihimize watu watoke kwenda nchi tofauti duniani kutafuta maisha huko,viwandani,mashambani,mahotelin,madereva,mafundi,migodini,wauguzi,na wengine kutangaza utamaduni,lugha ya kiswahilii nk..kama walivyozagaa mataifa ya wenzetu duniani hususan wakenya,Nigerians nk
Yakifanyika haya kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira litapungua
Nawasilisha.