Vijana acheni kuoa watu wenye jinsia ya kike, oeni wanawake

Vijana acheni kuoa watu wenye jinsia ya kike, oeni wanawake

kichomiz

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
20,360
Reaction score
13,465
Habari zenu wana Jamii Forums

Twende moja kwa moja kwenye mada, Vijana wa leo wamekuwa wakurupukaji na malimbukeni,kwenye swala kuoa
Wamejikuta wakioa watu wenye jinsia za kike na si wanawake, matokeo yake kuyumbishwa, kupelekeshwa na kurudishwa nyuma kiuchumi.

Wengi huendeshwa na tamaa na kufata mkumbowatu wenye jinsia za kike ni pasua kichwa:
(1) Ni wajuaji wa kila kitu
(2) Wamejaa viburi na majivuno
(3) Si wasikilizaji ila ni waropokaji wazuri sana
(4) Wana lugha chafu midomoni mwao na wapenda shari
(5) Wanapenda kulazimisha wafanyiwe vitu hata kama huna uwezo nacho

Ukiwa na huyo mtu mwenye jinsia ya kike, tegemea kurudi nyuma kiuchumi kwa %99 na kupata magonjwa ya ajabu ajabu

images-19.jpg

Sasa kwa nini kijana mdogo ujiingize kwenye matatizo yanayoepukika? Unakuta kijana mdogo wa umri wa 25 /30 , anahangaika na matatizo ya mahusiano badala ya kuhangaika na kujijenga kiuchumi

Kichwa cha mwanaume huwa hakitaki kelele, kinataka utulivu ili kupanga na kuchakata mipango endelevu ya maendeleo

METHALI 21:19
 
Inawezekana sijakuelewa mwandishi. Una maana wanaume waoe wanaume wenzao???
 
Ni kwa nini umepeleka mawazo yako huko?

Wengi huendeshwa na tamaa na kufata mkumbowatu wenye jinsia za kike ni pasua kichwa:
......... wakioa watu wenye jinsia za kike na si wanawake

Hizo sentesi hapo juu ndio zimepelekea mimi kuwa na mawazo hayo na nikaamua kuhoji
 
Dah ndio mana hujaelewa kwa sababu ya uvivu
 
Hizo lugha chafu huwa zinanichefua kwakweli, alaf wao wanaona ujanja kweli
Kuna mmoja nilikuwa naye majuzi akaropoka "hawa voda siku hizi wamekuwa wase.nge"..kisa tu vi-mb vyake vimeisha fasta, nikawaza huyu si kuna siku na mimi ataniporokoshea hizo lugha chafu.
 
Back
Top Bottom