Vijana acheni kuwekeza sana kwenye decorations za duka badala ya stock

Kuna watu wanauza trust na aesthetics kwenye hiyo biashara, wengi wao wauza simu. Huwezi uza iPhones kwenye duka lenye sakafu na mabenchi wateja hawatoamini kama hata warranty watapata.
Huu uzi sio sheria. Ni ushauri tu. Kama huu ushauri hauendani na biashara yako inavyotaka basi ni vyema na sahihi kutoufuata
 
Uzi mzuri sana kwa wambanaji way back kuna jamaa yangu mmoja alifungua saloon mtaani nimemwambia ifanye iwe simple maan bado ramani ya mchezo hujaujua bado jamaa akawa mbishi akaipiga tyris fresh kuanzia ndani ukutani kote mpaka nnje kote kilicho mkuta ni balaa biashala akachemka akaondoka akaacha kamnufaisha mwenye frem
 
kuna baadhi ya biashara branding ni muhimu kuliko product yenyewe inaleta trust na sense of pride kwa wateja sasa wewe leta pigo za kiduanzi ofis kama chimbo la halmashauri kwenye biashara za kitozi uone utakavyoshinda kwa waganga
 
Huu uzi sio sheria. Ni ushauri tu. Kama huu ushauri hauendani na biashara yako inavyotaka basi ni vyema na sahihi kutoufuata
Umepanick, hakuna nilipodai uzi ni sheria. Labda useme umejiandikia mwenyewe kwamba watu wasichangie. Si lazima kila mtu awe na mtazamo wako, mtazamo wangu na wako ni tofauti.

Inategemea na biashara, kuna maduka mengi ya vijana yanauza kwa mali kauli. Anaweka nguvu kwenye marketing na aesthetics maana mtaji haufanyi lolote kwenye inventory. Na wanauza sana tu sometimes kupita wenye maduka. Biashara halijawahi kuwa suala la kukaririshwa. Ever-changing business environment
 
Punguza uoga
 
Umeweka mabango ya tigopesa, airtel money, mpesa, Crdb, nmb nk tena mabango makubwa. Halafu mtu anakuja kuhitaji huduma ya crdb unamwambia bado hatuna mashine. Hii ipo sana, decorating an office ni gharama kubwa sana, japo kuna ofisi bila decorations haiuzi.
 
Decoration au branding ni sehemu ya mtaji mkuu kuna biashara lazima ufanye rebranding kuendena na biashara yako mada yako haija taja biashara ya aina gani isio hitaji decoration kali.....acha ku generalise mkuu.
 
Mkuu tofautisha decorating and advertising hivi ni vitu viwili tofauti, kutangaza huduma usio nao kunauua huduma hata zingine ata ulizo nazo.
 
Decoration au branding ni sehemu ya mtaji mkuu kuna biashara lazima ufanye rebranding kuendena na biashara yako mada yako haija taja biashara ya aina gani isio hitaji decoration kali.....acha ku generalise mkuu.
Ni ushauri tu sio lazima kuufuata
 
Mfano mzuri sana huu.. juzi nilikua natafuta saloon ya kunyoa.. kila saloon nikiiona naona hii ni zile saloon za kishua kunyoa 10,000. Sababu ya decoration na madoido waliyoweka.. siingii saloon hizo.. nkatafuta mpaka nkaona saloon zile za kawaida ndo nkaingia..
 
Mkuu bango linatengenezwa kwa gharama, mtu hana hela ya kuchezea eti aweke Tigopesa na M-Pesa tu miezi mitatu baadae akiweka na CRDB achane bango aweke bango jipya.

Sometimes mtu anaweka tangazo la vitu kadhaa ambavyo hawezi kuvimudu vyote kwa pamoja ili aangalie feedback, kipi kinaulizwa zaidi ndio akianzishe kabla ya vingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…