Vijana acheni kuwekeza sana kwenye decorations za duka badala ya stock

Vijana acheni kuwekeza sana kwenye decorations za duka badala ya stock

Sasa zile ni decoration au bidhaa we nawe yani izo izobidhaa ndo wanafanyia decoration
Unawasema wauza nyanya na mifuko ya plastiki si ndio? Sasa decorations kwenye banda la nyanya ya nini. Tafuta Wachaga wauza electronics, accessories & gadgets uone kama hawajafanya decorations
 
Mojawapo ya kosa kubwa sana la kiufundi kwa vijana wengi wadogo wanaoanza biashara ni kuwekeza pesa nyingi kwenye vitu ambavyo havirudishi pesa kwa haraka au pengine havirudishi kabisa. Vijana wanafungua maduka ila wengie hawafikishi mwaka mmoja wamefunga baada ya kushindwa biashara.

Vijana wanafanya makosa mbalimbali ya kiufundi ila kosa lililoshika kasi zaidi ni kutumia pesa nyingi sana kufanya decorations ya duka badala ya kununua mzigo wa kutosha. Imekuwa kawaida kuona bajeti ya decorations milioni 5 halafu mzigo wa dukani milioni 3. Ukiliona duka kwa nje ni zuri balaa hadi ndani ila mzigo ni mdogo usioendana na hadhi ya duka. Wengine hufanga kosa zaidi kwa kuteketeza pesa kufanya sherehe ya uzinduzi wa duka (launching party).

Ninawashauri vijana wakiwa wanafungua duka wafanye decorations za kiasi kidogo sana ila baadae wakijaliwa watafanya decorations kali kwa kutumia sehemu ya faida iliyopatikana kwenye biashara. Vijana acheni kushangilia ushindi wakati hata mechi bado. Hakikisheni mnanunua stock ya kutosha. Huo ndo usalama wa biashara.
Sio kila anayefungua duka ni muuza duka watu wana minuo zao duka ni kuzuga tu kama uhamini njoo sinza uone mabalaa huku..
 
Hizo decoration wakati fulani zinaweza kuwakimbiza wateja wakihisi kwa uwezo wao hawawezi kununua bidhaa zilizomo kwa kudhani bei itakuwa ghali sana, kuna bucha fulani lilifunguliwa limefanyiwa decorations za kufa mtu mpk unahisi humu kweli nikitaka nyama robo wanapima kweli!! Au bei yake ndiyo hii sawa na bucha za kawaida

Basi inabidi ulipite tu uende bucha za kawaida hizi mpk walipobandika bei ndiyo mtu anafahamu kumbe bei sawa tu ni mbwembwe tu decorations hata wanyonge wanaweza kuingia
Sometimes muonekano unatishia, unaeza ona duka lipo decorated sana ukaogopa ukidhani bei nazo zitakuwa na hadhi ya muonekano kumbe sio.
 
VIJANA WATULIZE SANA AKILI KWENYE BIASHARA, BADO WANA DANGANYWA SANA WALIO KWENYE BIASHARA PIA ISITOSHE NA WAO PIA WANAJIDANGANYA!
 
Kuna kitu sisi vijana wengi tunapotezwa sana decoration inatakiwa kuwa ya kawaida very simple but with elegant design sasa wengi inakuwa ndo mtu anaanza biashara anaweka mbwembwe nyingi hapo tutapoteana . Pia renovation inaweza kufanyika kila baada ya mda flan
 
Umepanick, hakuna nilipodai uzi ni sheria. Labda useme umejiandikia mwenyewe kwamba watu wasichangie. Si lazima kila mtu awe na mtazamo wako, mtazamo wangu na wako ni tofauti.

Inategemea na biashara, kuna maduka mengi ya vijana yanauza kwa mali kauli. Anaweka nguvu kwenye marketing na aesthetics maana mtaji haufanyi lolote kwenye inventory. Na wanauza sana tu sometimes kupita wenye maduka. Biashara halijawahi kuwa suala la kukaririshwa. Ever-changing business environment
amepanic kivipi wakati amekwambia "Kama huu ushauri hauendani na biashara yako inavyotaka basi ni vyema na sahihi kutoufuata" au we unajibu lako unataka akupe?
 
Ninayo app nzuri ya kupiga mahesabu ya duka.Inafaa kutumia wakati wa kufanya stock.
1.Unaweza kujua duka lako limekuingizia sh. kwa mwezi au kwa mwaka.
2. Inaonyesha thamani stock iliyopo dukani
3. Inaonyesha Kila bidhaa unayouza Ina faida ya sh. ngapi
4. Kama Kuna upotevu wa fedha inaonyesha.

INAFAA KUTUMIA KWENYE SMART PHONE AU COMPUTER

Ili kuitumia unatakiwa kuwa na rekodi sahihi za Kila manunuzi na mauzo ya Kila siku. Nicheki Whatsapp 0753546162
 
umeshindwa kueleza vizuri tu mkuu..inategemea biashara unayoifanya unauza bidhaa zinazodeal na decoration then dukani kwako pawe pa hovyo hovyo kweli??.
Hajasema usifanye decorations kabisa, kasema unafanya kiasi tu kwa kua ndio unaanza, baadae sasa ndo unafany kwa kutumia sehem ya faida unayopata
 
Back
Top Bottom