Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Vijana acheni pombe na Energy drinks, mwifwa

Ndo ukweli huo. Tafuta gazeti la Mwananchi la jana Machi 15, 2024 wameandika kwa kina sana...inaonekana unywaji pombe ni tatizo sana hasa kwa Vijana, ushahidi ni ukienda wikiendi Tabata, Kitambaa, Rainbow etc
Hii shisha ndo tatizo kabisa. Ushahidi wa Kisayansi unaonesha uvutaji wa shisha prolonged unasababisha Kansa ya mapafu, utumbo, kansa ya kibofu, na kansa iitwayo nasopharyngeal aka kansa ya koo.
 
Aisee Mimi bila Energy drinks sijisikii vizuri kabisaaa, 2014 nilikuwa nakunywa mpaka 6 per day lakini Sasa hivi asubuhi kabla sijala chochote lazima ninywe moja baridiii sana ndio nitafute chai Sasa. 🤣🤣🤣
Madhara yake utayapata baada ya miaka 10-15 ijayo. Sasa hivi bado una mwili strong unaweza kupokea mapigo yoyote,
 
Nimesoma gazeti la Mwananchi jana lenye kichwa cha Habari ukurasa wa mbele kisemacho
Pombe, 'energy drinks' zinavyomaliza vijana

Kwa mujibu wa hili gazeti wakinukuu wataalamu wa afya wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma ni kwamba:-

1. Vijana Wanne hadi Tisa hufika Hospital hiyo kila wiki Figo zikishindwa kufanya kazi.

2. Watanzania 10 kati ya 100 wana tatizo la Figo

3. Wahanga ni vijana umri kati ya 24-40

4. Gharama za kusafisha Figo kwa mwaka ni wastani wa TZS 31,200,000 Hadi 46,800,000 bila kuweka gharama nyingine kv usafiri

5. Energy drinks ni disaster kwenye moyo kwa mujibu daktari bingwa wa JKCI.

6. Matumizi ya vinywaji hivi yanaathiri pakubwa viungo vitatu ambavyo ni
-Ini,
- Figo na
- Moyo.

7. Wahanga wakubwa ni vijana wa kiume.

MY TAKE:

Vijana acheni pombe, taifa linawategemea. Linda afya yako. Afya ni mtaji.
Mbona Hayo Matatizo Tunayaona Kwa Wazee Si Vijana?

Tuzingatie Afya Katika Ulaji Wetu
 
Back
Top Bottom