Vijana BAVICHA Pwani wamtaka John Heche apishe uchunguzi

Vijana BAVICHA Pwani wamtaka John Heche apishe uchunguzi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Aliyejitambulisha kama Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Pwani, Ramadhan Mwaja, amesema Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, apisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili ambazo zimekuwa zikijadiliwa katika mitandao ya kijamii, akisema hatua hiyo itasaidia kutoa nafasi kwa mamlaka husika kufanya uchunguzi kwa uhuru ili ukweli ubainike.

"Lengo letu si kumhukumu mtu yeyote, bali ni kukinusuru Chama. Tunataka mamlaka zifanye kazi yake, na mwisho wa uchunguzi ukweli ujulikane," alisema.

Ramadhan alisema endapo hatua hiyo haitachukuliwa, Chama kinaweza kuendelea kukabiliwa na maswali kutoka kwa wanachama na wananchi kuhusu tuhuma hizo, jambo ambalo linaweza kuathiri taswira yake.

Aidha, alisema wakati wa uchaguzi kulikuwa na ahadi kwamba fedha za ujenzi wa Chama zingeshushwa hadi ngazi ya majimbo kila mwezi ili kuimarisha shughuli za Chama. Hata hivyo, alidai kuwa hadi sasa fedha hizo hazijawafikia viongozi wa majimbo kama ilivyoahidiwa.

"Nikiwa Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Pwani, nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa viongozi na wanachama kuhusu fedha hizo, lakini hatuna majibu ya kutoa. Hali hiyo inaleta sintofahamu na kuathiri utekelezaji wa shughuli za Chama," alisema.

Aliongeza kuwa iwapo kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wa ahadi hiyo, ni muhimu uongozi wa Chama utoe maelezo ya wazi kwa wanachama ili kuondoa mashaka yaliyopo.

Tamko hilo limetolewa na vijana wa BAVICHA Mkoa wa Pwani wakisema linalenga kuimarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na uadilifu ndani ya Chama, huku wakisisitiza kuwa ukweli kuhusu tuhuma zinazojadiliwa unapaswa kubainishwa kupitia uchunguzi wa mamlaka husika.

Soma Pia:
 
Maelezo yaliyopo hapa yana ukakasi.

Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Umoja wa Vijana wa Chama hicho (BAVICHA) Mkoa wa Pwani wamemtaka Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Mheshimiwa John Heche, kupisha uchunguzi unaohusiana na tuhuma zinazomkabili ambazo zimekuwa zikijadiliwa katika mitandao ya kijamii.

heche ni mwenyekiti wa bavicha ?
 
Aidha, alisema wakati wa uchaguzi kulikuwa na ahadi kwamba fedha za ujenzi wa Chama zingeshushwa hadi ngazi ya majimbo kila mwezi ili kuimarisha shughuli za Chama. Hata hivyo, alidai kuwa hadi sasa fedha hizo hazijawafikia viongozi wa majimbo kama ilivyoahidiwa.
Shida iko hapa.........
 
Wakati CHAMA kimefungiwa kufanya kazi vijana kama hawa walikuwa kimya.

Sasa kimefunguliwa na pesa zimeana kuingia basi Vijana wametaka hela.

Vijana wa namna hii hawafai katika uongozi.

Mwisho anaomba SAMIA - mtukufu.. hapa kalipia tangazo kwa kumtaja mdhamini.
 
Wakati CHAMA kimefungiwa kufanya kazi vijana kama hawa walikuwa kimya.

Sasa kimefunguliwa na pesa zimeana kuingia basi Vijana wametaka hela.

Vijana wa namna hii hawafai katika uongozi.

Mwisho anaomba SAMIA - mtukufu.. hapa kalipia tangazo kwa kumtaja mdhamini.
Hata muhalifu angekuwa na akili nyingi na njema kiasi gani, lazima ataacha ushahidi/alama za uhalifu wake.Huwa ni suala la umakini wa mfuatiliaji au muda tu.Huo mwisho ndiyo an alibi/kidhibiti sahihi kwa upuuziupuuzi wao wa kupewa peremende na kubugia tu bila kujua zina sumu.
 
Huyo Katibu mjinga anataka fedha za ujenzi wa chama zisishwe mpaka chini kutoka wapi?

Aende akamuulize msajili kwanini Chadema haipewi ruzuku.
Ni ahadi iliyotolewa na uongozi ulio madarakani. Mapato ya Chama hayatokani na ruzuku peke yake. Kuna ada, michango ya wananchi n.k. Uongozi ulipaswa kuwaambia viongozi wao wa chini kwa nini ahadi hiyo haitekelezeki kwa sasa. Ndio umuhimu wa uwazi katika taarifa za makusanyo na matumizi ya chama.

Amandla...
 
Chama hichi kinapitia mengi, hata wasio na chama wanaanza kukionea huruma huku wakijua huu ni uonevu
Kwenye hivi vyama hasa vya ukinzani bila umakini watasumbuliwa sana tu.Ile kanuni/sheria ya uanzishwaji wa vyama kutaka kila wilaya chama kiwe na uwakilishi ni chanzo kikuu cha kupokea mamluki na wasaka tonge.Kuna wilaya/mikoa ukisikia chama fulani kina uongozi na wanachama lazima ucheke hadi machozi.
 
Back
Top Bottom