Vijana BAVICHA Pwani wamtaka John Heche apishe uchunguzi

Kwenye hivi vyama hasa vya ukinzani bila umakini watasumbuliwa sana tu.Ile kanuni/sheria ya uanzishwaji wa vyama kutaka kila wilaya chama kiwe na uwakilishi ni chanzo kikuu cha kupokea mamluki na wasaka tonge.Kuna wilaya/mikoa ukisikia chama fulani kina uongozi na wanachama lazima ucheke hadi machozi.
Bila kuweka viongozi kuanzia ngazi ya wilaya/mikoa kuna maeneo watashindwa kuwafikia wananchi wao. Shida inakuwa wanaposajili mamluki, hawa hawakwepeki, wanapaswa kuwachukulia hatua haraka.
 
Njia ya kuelekea kwenye maridhiano na CHADEMA imeshindikana na sasa CCM inatumia pesa nyingi Sana kumwondoa Heche madarakani..
Mbinu za kizamani sanaa hizi CCM wanatumia , hii Ndiyo mbinu ya mwisho iliyobaki ndani ya CCM na mwisho wa siku itabuma tu
 
Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Umoja wa Vijana wa Chama hicho (BAVICHA) Mkoa wa Pwani wamemtaka Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Mheshimiwa John Heche, kupisha uchunguzi unaohusiana na tuhuma zinazomkabili ambazo zimekuwa zikijadiliwa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwa niaba ya vijana wa BAVICHA Mkoa wa Pwani, Katibu wa BAVICHA Mkoa huo, Ndugu Ramadhan Mwaja, alisema hatua hiyo itazipa mamlaka husika nafasi ya kufanya uchunguzi kwa uhuru ili ukweli ubainike.

"Lengo letu si kumhukumu mtu yeyote, bali ni kukinusuru Chama. Tunataka mamlaka zifanye kazi yake, na mwisho wa uchunguzi ukweli ujulikane," alisema.

Ramadhan alisema endapo hatua hiyo haitachukuliwa, Chama kinaweza kuendelea kukabiliwa na maswali kutoka kwa wanachama na wananchi kuhusu tuhuma hizo, jambo ambalo linaweza kuathiri taswira yake.

Aidha, alisema wakati wa uchaguzi kulikuwa na ahadi kwamba fedha za ujenzi wa Chama zingeshushwa hadi ngazi ya majimbo kila mwezi ili kuimarisha shughuli za Chama. Hata hivyo, alidai kuwa hadi sasa fedha hizo hazijawafikia viongozi wa majimbo kama ilivyoahidiwa.

"Nikiwa Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Pwani, nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa viongozi na wanachama kuhusu fedha hizo, lakini hatuna majibu ya kutoa. Hali hiyo inaleta sintofahamu na kuathiri utekelezaji wa shughuli za Chama," alisema.

Aliongeza kuwa iwapo kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wa ahadi hiyo, ni muhimu uongozi wa Chama utoe maelezo ya wazi kwa wanachama ili kuondoa mashaka yaliyopo.

Tamko hilo limetolewa na vijana wa BAVICHA Mkoa wa Pwani wakisema linalenga kuimarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na uadilifu ndani ya Chama, huku wakisisitiza kuwa ukweli kuhusu tuhuma zinazojadiliwa unapaswa kubainishwa kupitia uchunguzi wa mamlaka husika.

Soma Pia:
Boni Yai( kijana wa mbowe)... ndie mwenyekiti wa kanda hii ya pwani...

Boni yai(ex mayor ubungo) na MMM Martin maranja masese...HAWA NI VIJANA WATIIFU WA MBOWE!

Mbowe ataacha lini chokochoko hizi?!

ADUI NAMBA MOJA WA SIASA ZA HILI TAIFA NI KIKWETE NA MBOWE! Kataa ,ukubali, ni juu yako!
 
Fukuzeni wote siku chadema ikijua nguvu iliyonayo kwa wananchi wafukuza hawa wote mamuluki
 
Fukuzeni wote siku chadema ikijua nguvu iliyonayo kwa wananchi wafukuza hawa wote mamuluki
 
Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Umoja wa Vijana wa Chama hicho (BAVICHA) Mkoa wa Pwani wamemtaka Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, Mheshimiwa John Heche, kupisha uchunguzi unaohusiana na tuhuma zinazomkabili ambazo zimekuwa zikijadiliwa katika mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwa niaba ya vijana wa BAVICHA Mkoa wa Pwani, Katibu wa BAVICHA Mkoa huo, Ndugu Ramadhan Mwaja, alisema hatua hiyo itazipa mamlaka husika nafasi ya kufanya uchunguzi kwa uhuru ili ukweli ubainike.

"Lengo letu si kumhukumu mtu yeyote, bali ni kukinusuru Chama. Tunataka mamlaka zifanye kazi yake, na mwisho wa uchunguzi ukweli ujulikane," alisema.

Ramadhan alisema endapo hatua hiyo haitachukuliwa, Chama kinaweza kuendelea kukabiliwa na maswali kutoka kwa wanachama na wananchi kuhusu tuhuma hizo, jambo ambalo linaweza kuathiri taswira yake.

Aidha, alisema wakati wa uchaguzi kulikuwa na ahadi kwamba fedha za ujenzi wa Chama zingeshushwa hadi ngazi ya majimbo kila mwezi ili kuimarisha shughuli za Chama. Hata hivyo, alidai kuwa hadi sasa fedha hizo hazijawafikia viongozi wa majimbo kama ilivyoahidiwa.

"Nikiwa Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Pwani, nimekuwa nikipokea maswali mengi kutoka kwa viongozi na wanachama kuhusu fedha hizo, lakini hatuna majibu ya kutoa. Hali hiyo inaleta sintofahamu na kuathiri utekelezaji wa shughuli za Chama," alisema.

Aliongeza kuwa iwapo kutakuwa na changamoto katika utekelezaji wa ahadi hiyo, ni muhimu uongozi wa Chama utoe maelezo ya wazi kwa wanachama ili kuondoa mashaka yaliyopo.

Tamko hilo limetolewa na vijana wa BAVICHA Mkoa wa Pwani wakisema linalenga kuimarisha misingi ya uwazi, uwajibikaji na uadilifu ndani ya Chama, huku wakisisitiza kuwa ukweli kuhusu tuhuma zinazojadiliwa unapaswa kubainishwa kupitia uchunguzi wa mamlaka husika.

Soma Pia:
sidhani kama atafikisha saa 10 jioni huyo 🤣
 
Mkuu Waufukweni
Nadhani tusijaze serva za Jamii Forum bila sababu za Msingi.

Kulikuwa na mambo mengi tu ya hao watu kuja Front.
1. Utekaji.
2. Mauaji.
3. Kesi ya Lissu.
4. Commonwealth.
5. Katiba.
6. Tume huru ya Uchaguzi nk.

Wameambiwa kam wana hoja za msingi kuhusu hela za Tone tone wawasilishe Kwenye Uongozi makao makuu.

UNAJAZA SERVA BILA SABABU ZA MSINGI.
 
Tuliwaambia huyo TAKATAKA selasini mnamuingiza ndani ya CHADEMA na wapumbavu wenzake watakuja kuleta vurumai mkadhania anasingiziwa,huyo hapo sasa ameanza habari zake. Huyu mzee ni mtaalamu wa fitina na anajua kuchonganisha wanachama kupita maelezo.
 
Madelu + CCM/ unapata 30 + bavicha wa mchongo / upumbavu CCM inajinyea huku inatembea aibu
 
Back
Top Bottom