Vijana fuateni ushauri wa waziri mkuu Majaliwa kuhusu ajira

Vijana fuateni ushauri wa waziri mkuu Majaliwa kuhusu ajira

Ndinani

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2010
Posts
7,329
Reaction score
4,286
Nimemsikia waziri mkuu Kassim Majaliwa Juzi akiwa Shauri vijana wenye shahada za vyuo vikuu lakini hawana ajira wajiunge na vyuo vyetu vya Veta ili kujifunza SKILLS mbali mbali.

Nimesoma pia kwenye mitandao vijana wakiubeza ushauri huu!! Ushauri huu ni mzuri ambao vijana wanatakiwa kuuchangamkia badala ya kuzunguka na bahasha za certificates kutafuta kazi maofisini! Ukiwa na shahada yako ukaenda VETA ukajifunza jinsi ya kutengeneza/repair engine za magari au matrekta ni dhahiri kuwa ukihitimu huwezi kukosa kazi ya kuendesha maisha yako ; hasa wakati huu ambao serikali onahimiza agricultural mechanization. Huko mashambani mafundi wa kurepair matrekta na mitambo mwingine watahitajika sana.

Veta wanafundisha fani nyingi kama mambo yanayohusu umeme, mambo yanayohusu computers, urembo, mapishi, uselemala etc. Given background ya hawa vijana wenye shahada itakuwa rahisi kwao kuhitimu kwenye hizo fani kwa muda mfupi na kuanza kupata kipato.

Dunia ya leo ili kufanikiwa watu hutegemea sana SKILLs kuliko degree certificates. Mtu mwenye ujuzi wake awe fundi bomba au Seremala hawezi kulala na njaa kwani huduma zao zinahitajika na wengi na kila mara!

Soma Waziri Mkuu Majaliwa: Wenye degree kasomeni ufundi VETA mjiajiri
 
Alafu utakuwa wew ni mtu unaeheshimika mtaani eti una post such a sh*t!
 
Matusi haya kwa Vyuo Viku
Matusi haya kwa Vyuo Vikuu
Sio matusi tu kwa vyuo vikuu bali mfumo wetu wote wa elimu! Tunafundisha watoto wetu toka elimu ya chini mpaka chuo kikuu ili wakaajiliwe!! Elimu ya sasa hata hao wanaohitimu vyuo vikuu hailengi mahitaji ya soko hivyo wakihitimu hukosa ajira!
 
Matusi haya kwa Vyuo Vikuu
Sio lazima,kaa na cheti chako mtaani usubiri kuajiriwa.Kuna dada namfahamu ana masters degree huu ni mwaka wa 15 hana ajira,kajiongeza anauza vitenge na nguo za kutembeza mtaani...
 
Tupike mwaya.. watu hawaachagi kula 🤣
Huo ndo ukweli sina cheti Cha mapishi Ila Swahili foods nikitengeneza ni moto,

Assume watoto wa NCT mm walikuwa wanapata ujuzi toka kwangu 😂

Hizi international ndo siijui Ila vya kibongo aweh!

Juzi Kuna mtu kaomba nimpikie order 😂 ety hajui kupika roast la nyama mix njegere,
 
Ni mazishi au mapishi? Hebu rekebisha hilo neno. Unajua hawa vijana ni wapuuzi na wajinga hawaoni fursa za ajira, wanadhani shahada zao zitawapa ajira maofisini wakipulizwa na upepo mwanana wa feni na kiyoyozi, hawataki kupigwa jua, kulizwa na upepo mkali, kuchafuka na grisi, oili, rangi, vumbi, udongo, matope, kulowa maji. Ni mentality ya kipumbavu kudhani degree itakupa ajira nyororo yenye ukwasi mwingi, ni ujinga kuipa degree hadhi ya utukufu kwamba ukiwa nayo utapata kila kitu bwerere without action, mind that skilled labour is the future of Tanzania. Vijana wenye degree nendeni VETA mkasome ufundi mpate ujuzi na maarifa ya kujiajiri. Kwa kuwa mna sifa za kuwa na shahada ikitokea nafasi huko mnapotaka muajiriwe mtaajiriwa kwa mujibu wa sifa mlizonazo kuliko kukaakaa jobless na kuwa na misongo ya mawazo. Mna elimu kubwa lakini mnashindwa kuona fursa na kutatua shida zenu, huko ni kurutubisha ufukara na umasikini, badilisheni mindset, shwaini, mlienda shule kusomea ujinga?
 
Napiga zangu paints and Aluminum fittings..hapo nimemaliza Plumbing ile ya 6Months...
Nitajiegesha hapo Dodoma na Mbeya..
 
Back
Top Bottom