Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Geita Mjini, Ndaro Samsoni, amewahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kupiga kura litakalofanyika Oktoba 29 mwaka huu ili kuchagua rais, mbunge na diwani. Ndaro amesema ushiriki wa vijana ni muhimu kwa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu, ili viongozi watakaopatikana wawe ni chaguo la wananchi.
Amefafanua kuwa mikutano ya uhamasishaji imekuwa ikitumiwa kuwahimiza vijana kutumia haki yao ya kikatiba na kuchagua viongozi wanaowataka.
Aidha, amesema juhudi za uelimishaji zinaendelea kupitia vyombo vya habari na kampeni za jamii, zikiwa na lengo la kuwafikia wananchi wote bila ubaguzi. Ndaro ameongeza kuwa iwapo vijana watajitokeza kwa wingi, Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 utakuwa na mafanikio makubwa.