Nimekuwa nikifatilia uchaguzi wa chama cha mapinduzi (CCM), Na Mzee Wasira amefanikiwa kupita kuwa makamu mwenyekiti. Sina ubaya na mzee Wasira(80). Ila swali langu kuwa vijana wamekosa nini au wana dhambi gani hadi wasiaminiwe.
Kila siku wazee wanawaambia vijana wajiajiri huku wenyewe waking'ang'ania ofisi mfano huyu mzee miaka themanini ila amerudi kuajiriwa na chama.
Sasa vijana wenzangu tukae tukijua adui wa vijana ni wazee hawatulio nao.