Vijana kachukueni Pasipoti zenu Uhamiaji mtawanyike Duniani; kusubiri ajira na uteuzi ni utumwa wa fikra

Vijana kachukueni Pasipoti zenu Uhamiaji mtawanyike Duniani; kusubiri ajira na uteuzi ni utumwa wa fikra

Vijana wa Sasa hivi siyo wasafiri Kama vijana wa zamani, Vijana wa siku hizi akipata pesa kidogo tu anakimbilia kununuwa godoro na kabati, Sasa huyu ukimwambia kuhusu safari,anaanza kuwaza godoro lake na kabati atamuachia nani!?
Very correct
 
Kwa jinsi tulivyo wavivu, hatutoweza kuishi nchi za wenzetu.
Sisi ngoja tuendelee tu kuishi hapa hapa bongo tukishinda kwenye vijiwe vya kahawa huku tunabishana issue za simba na yanga.
Wewe na machoko wenzako inatakiwa muuzwe nnje ya nchi kama mbolea..
 
Mhe. RAIS ameifungua nchi, SI Kwa wazee Bali Kwa vijana. Wakenya wamejaa Tanzania Kwa ajili ya matembezi ,biashara, ajira nk. Sisi Watanzania tumejazana Dar na tunajipongeza Kwamba tumeiona Dunia. Hapana vijana badilisheni fikra, mtizamo na mikakati, wazeni kuvuka mpaka, wazeni kufanya biashara za kuvuka mpaka, wazeni kuajiriwa Duniani.

Mnatafuta distinction za Nini kama fikra zimeishia dar? Maisha ya Dar ndiyo yakufanye usote ukisoma bila kulala? Unapata first class anateuliwa lower second? Unapata first class ujui hata mwonekano wa passport, hapana tukatae utumwa tutembee tuache mji upumue.

Naandika haya baada yakuona tatizo la ajira nchini, hakuna namna utumishi wa umma ulio na uwezo wa kuajiri less than one milioni utafanikisha kiu ya wataka ajira. Acheni kupoteza muda, ondoeni fikra za kupata life Tanzania pekee wazeni nje.

Vijana wakitoka Kwa wingi watapata ujira nje na kutuma fedha zitakazotumika kama mitaji Kwa ndugu zao , vijana wakitoka Watanzania watapata pakufikia HUKO nje. Tutoke

Dar imejaa kila mwanafamilia nchi Hii, hakuna mwenye hofu ntafikia wapi dar maana kila Kijiji kina mtu dar, kwanini tusiamue kuwa na mwanafamilia kila mji Duniani? Tunaweza tuanze Sasa. Tutoke

Tumfate Mkuu wa Uhamiaji atupe pasipoti zetu ambazo amekabidhiwa akae nazo akisubiri tufike watupe, tumpunguzie jam mama Samia Kwa kusambaa kuliko Sasa kila wakati tunampigia kelele atuajiri. Tutoke.

Kama tulivyo wakarimu ndivyo na wenzetu walivyo, tuondoe hofu maana Mabalozi wapo Duniani kote wanalipwa fedha kutulinda tunapoonewa. Tutoke.

Kampeni Hii iwe chachu ya watawala kuwakumbusha vijana wajibu wao wa kutoka , iwe kampeni ya vyuo kutoa elimu ya kujitegemea HUKO nje, ndani tumejaa. Iwe kampeni ya nchi katika kukuza Diplomasia na kupanua mapato yatokanayo na Watanzania waishio nje. Tutoke.

Tunao madaktari na Manesi, tunao vijana wa IT ambao kwa wingi wao tumeshindwa kuwaajiri. Tuwasaidie watoke wakafanye kazi nje mwisho tutawaita wakiwa tayari wamebobea na nimadaktari bingwa. Vijana tokeni

Yaani kama wanigeria tu, kila kona wapo
 
Mimi nilifatilia mpaka nikachoka nikaahilisha, nikaona acha tupapalikie huu huu mkate mdogo uliopo hapa kwetu
 
Kuna watu wanachukulia kila kitu easy kupata passport Tanzania sio rahisi kama mnavyofikiria kama ww ulipata ki urahisi basi ilikuwa bahati yko tu ila wale wanapenda hela kama hawalipwi mishahara.
 
Ukishakuwa na kitambulisho cha kuzaliwa au cha uraia upewe passport yako.....
Sasa vyeti vya kuzaliwa vya wazazi navitoa wapi sasa hivi
 
Kutoka thd za kuponda wabeba box mpaka thd za kushauriana kutafuta fursa za kwenda kubeba box nje,

Kweli muda ni muamuzi mzuri sana,
Nakomaa na box hapa kwa Malkia.
 
Back
Top Bottom