Vijana kachukueni Pasipoti zenu Uhamiaji mtawanyike Duniani; kusubiri ajira na uteuzi ni utumwa wa fikra

Vijana kachukueni Pasipoti zenu Uhamiaji mtawanyike Duniani; kusubiri ajira na uteuzi ni utumwa wa fikra

Kuna watu wanachukulia kila kitu easy kupata passport Tanzania sio rahisi kama mnavyofikiria kama ww ulipata ki urahisi basi ilikuwa bahati yko tu ila wale wanapenda hela kama hawalipwi mishahara.
Tafuta mtu wa kukutuma pale me nilipewa passport siku 2 trust me na sikuandika documents yoyote vyote waliandika wao wakiniuliza kwenye simu
 
Ukishakuwa na kitambulisho cha kuzaliwa au cha uraia upewe passport yako.....
Sasa vyeti vya kuzaliwa vya wazazi navitoa wapi sasa hivi
Andika affidavit itasimama kama vyeti vya wazazi
 
Tafuta mtu wa kukutuma pale me nilipewa passport siku 2 trust me na sikuandika documents yoyote vyote waliandika wao wakiniuliza kwenye simu
Mkuu mimi nilikuwa na documents zote na kila nilikamilisha ila nilichelewa kupata passport japo nilifanikiwa ila nilichelewa kuipata ww ulibahatika mkuu.
 
Mkuu mimi nilikuwa na documents zote na kila nilikamilisha ila nilichelewa kupata passport japo nilifanikiwa ila nilichelewa kuipata ww ulibahatika mkuu.
Tatzo pale watumishi wanajiona kutoa passport kama ni hisani yao hakuna nidhamu KILA mtu anataka tengeneza mazngra ya kupga pesa
 
Kutoka thd za kuponda wabeba box mpaka thd za kushauriana kutafuta fursa za kwenda kubeba box nje,

Kweli muda ni muamuzi mzuri sana,
Nakomaa na box hapa kwa Malkia.
Mkuu siyo kila homa ni malaria mambo yamebadilika...nipe na mm fursa nije hapo elimu degree na nauli ninayo ya kunifikisha shida ni mchongo wa kupata visa
 
Mhe. RAIS ameifungua nchi, SI Kwa wazee Bali Kwa vijana. Wakenya wamejaa Tanzania Kwa ajili ya matembezi ,biashara, ajira nk. Sisi Watanzania tumejazana Dar na tunajipongeza Kwamba tumeiona Dunia. Hapana vijana badilisheni fikra, mtizamo na mikakati, wazeni kuvuka mpaka, wazeni kufanya biashara za kuvuka mpaka, wazeni kuajiriwa Duniani.

Mnatafuta distinction za Nini kama fikra zimeishia dar? Maisha ya Dar ndiyo yakufanye usote ukisoma bila kulala? Unapata first class anateuliwa lower second? Unapata first class ujui hata mwonekano wa passport, hapana tukatae utumwa tutembee tuache mji upumue.

Naandika haya baada yakuona tatizo la ajira nchini, hakuna namna utumishi wa umma ulio na uwezo wa kuajiri less than one milioni utafanikisha kiu ya wataka ajira. Acheni kupoteza muda, ondoeni fikra za kupata life Tanzania pekee wazeni nje.

Vijana wakitoka Kwa wingi watapata ujira nje na kutuma fedha zitakazotumika kama mitaji Kwa ndugu zao , vijana wakitoka Watanzania watapata pakufikia HUKO nje. Tutoke

Dar imejaa kila mwanafamilia nchi Hii, hakuna mwenye hofu ntafikia wapi dar maana kila Kijiji kina mtu dar, kwanini tusiamue kuwa na mwanafamilia kila mji Duniani? Tunaweza tuanze Sasa. Tutoke

Tumfate Mkuu wa Uhamiaji atupe pasipoti zetu ambazo amekabidhiwa akae nazo akisubiri tufike watupe, tumpunguzie jam mama Samia Kwa kusambaa kuliko Sasa kila wakati tunampigia kelele atuajiri. Tutoke.

Kama tulivyo wakarimu ndivyo na wenzetu walivyo, tuondoe hofu maana Mabalozi wapo Duniani kote wanalipwa fedha kutulinda tunapoonewa. Tutoke.

Kampeni Hii iwe chachu ya watawala kuwakumbusha vijana wajibu wao wa kutoka , iwe kampeni ya vyuo kutoa elimu ya kujitegemea HUKO nje, ndani tumejaa. Iwe kampeni ya nchi katika kukuza Diplomasia na kupanua mapato yatokanayo na Watanzania waishio nje. Tutoke.

Tunao madaktari na Manesi, tunao vijana wa IT ambao kwa wingi wao tumeshindwa kuwaajiri. Tuwasaidie watoke wakafanye kazi nje mwisho tutawaita wakiwa tayari wamebobea na nimadaktari bingwa. Vijana tokeni
Mkuu wazo lako ni zuri ila huoni kuna haja sisi vijana kuchangamkia fursa zilizoko humu humu nchi mfano fursa za kilimo,ufugaji,biashara ndogo ndogo za kati na kubwa,uchimbaji wa madini (urithi wetu kabisa) kuliko kukimbilia nje
Nadhani its better tutoke (tuombe passport as you said) tukiwa na dira mfano tutoke tumezalisha mazao yetu na kuyaongezea thaman huko twende kwa ajili ya kutafuta soko eg ufuta huko Liwale au mazao ya ziwan mfano samaki toka ukerewe
Kingine kufika Dsm au majiji ya aina hio isiwe ndio kipimo cha mafanikio...
 
Kuna ndugu yangu kanyimwa passport kisa barua ya shule,
Hakumliza dhule so hana cheti eti kwanini, viambatanisho vingine vyote vipo
Tutatue hapo kwanza kisha ndio tupande ndege
 
Uhamiaji wanatakiwa kutoa passport kwa yeyote mwenye uraia halali wa Tanzania na anayeweza kulipia, maswali mengine yote ambayo huwa wanauliza hayana msingi.
Nchi unayokwenda ndio wanatakiwa kuuliza hayo maswali.
 
Back
Top Bottom