Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Vijana Kariakoo wanapotea sana, Serikali iingilie kati

Hii ni mara ya pili bon yai anaandika kuhusu wale vijana wa k.koo watano
Waliniuma sana nikaassume ndo kuna mdogo wangu

Je kuna mtu anajua lolote kuhusu wale vijana
 

Attachments

  • D070ACA1-3944-4309-9D19-4A6A41CD354B.png
    D070ACA1-3944-4309-9D19-4A6A41CD354B.png
    567.8 KB · Views: 10
Wengi wanaochangia wamemung'unya sana maneno kiasi asiyejua kinachoendelea hapati clue ya yanayotokea,vijana wanaopotea Kariakoo ni upande wa vitu kama simu laptop na tv na vitu mfanano wa hivyo pamoja na spare za magari.

Mimi nafanya biashara ya spare za magari,nyuma miaka saba nikiuza used kwanza Kariakoo kisha Ilala kule Lindi St so nikizungumza kwa upande huo nawajua vijana pamoja na watu wazima 11 wamepotea toka 2022 hadi leo hawajulikani walipo wa mwisho kwa upande huu walipotea wawili kwa pamoja mwaka jana mwezi wa tano na wote miaka ya nyuma wakati nafanya used walikuwa wanajihusisha sana na kununua vitu vilovyokuwa vikiibiwa kwenye magari ya watu wenyewe wakiita ”full",yaani gari inavunjwa kioo wanatoa lock wanachukua kuanzia dashboard show p/window switch radio side mirrors headrest nje wanang’oa taa zote bumpers nyuma na mbele kama mmiliki alisahau chochote cha thamani wanabeba so hawa jamaa walikuwa wanakaa pale mnada wa spare ulioungua moto nyuma ya Big Born p/station.

Jamaa walikuwa wanakula na askari wa Msimbazi na Central wakati fulani Mambosasa akiwa mkuu wa police Dar akalivalia njuga kwa kuwapa kitu kama offer (maana walikuwa wanajulikana kote police Msimbazi Stakishari Central Mabatini kwamba ndiyo wanaodhamini biashara hiyo hata picha zao zilibandikwa kutani) kwamba kuanzia pale hawana kesi ila wakiri kuacha mara moja mchezo huo kwani option iliyokuwa ifanyike baada ya kudhihirika wanaendelea na kazi hiyo ni kupotezwa moja kwa moja na kwamba jeshi la polisi halitakuwa na muda wa kwenda kutoa maelezo mahakamani,kilichoendelea wanakijua wenyewe baadae walipovunja hicho kiapo ndiyo wakapotea.

Baada ya hii ambush ndiyo matokeo tunayoyaona sasa wizi ule umepungua kama siyo kuisha kabisa nadhani hata Agrey baada ya wale watano kupotezwa kuna mabadiliko.
😁😁
 
Ogopa sana sehemu watu wanafanya biashara kwa mali kauli, hilo eneo jua hao watu wana mtandao na wanaaminiana sana sasa wewe ukienda na ujinga wako wa tamaa na kuwaona maboya ukataka kuwapiga aise watakushughulikia kikatili sana.

Vijana tuwe waaminifu na makini sana kwenye biashara za mali kauli.
 
Back
Top Bottom