Pre GE2025 Vijana kumchukulia Fomu ya Urais Rais Samia 2025

Pre GE2025 Vijana kumchukulia Fomu ya Urais Rais Samia 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mmeshaongea na Mungu kwamba mama ataiona kesho?

Uchawa unazidi mpaka mnakuwa kama makahaba.
Rais samia ni mpango wa Mungu mwenyewe na uweza wake Mwenyewe Mungu atamlinda Rais wetu na kumpatia afya njema na nguvu ya kuendelea kututumikia watanzania wote mpaka 2030
 
Sasa huwa unatafuta nini siku nzima kupigia debe mtu kama hutafuti ulaji,acha kutufanya watoto bwana
Sasa hata jinsi ya kutafuta ulaji kwenyewe hajui.

Ccm kupitia Jitegemee holdings company Ltd inamiliki migodi mikubwa ya coal mining huko mikoa ya kusini, kama yeye wa maana si aombe wampe hata kazi ya udereva mshahara laki nane kwa mwezi?

Hiki anachokifanya hapa ni bora hata ya demu aliyekosa ramani anayeuza K yake.
 
Rais samia ni mpango wa Mungu mwenyewe na uweza wake Mwenyewe Mungu atamlinda Rais wetu na kumpatia afya njema na nguvu ya kuendelea kututumikia watanzania wote mpaka 2030
Wewe unapayuka wenzako wanakula utamu wa Ccm migodini uko.

Fainali uzeeni, wewe endelea na ututsa tu hapa JF uone utakufikisha wapi.

Hao Green guard wenu ukiona uwaoni ujuwe wanakula shavu kulinda kwenye migodi ya Ccm mshahara mzuri kula kulala bure.

Wewe endelea kukatika mauno tu hapa JF wenzako SAA hizi wapo Instagram wanaselect warembo wazuri kwa pesa ya matunda ya Ccm.
 
Vijana kwa umoja wao kutoka maeneo mbalimbali nchini wameamua kuchanga hela kwa ajili ya kumchukulia Fomu ya urais mama Samia Mama wa shoka,chuma cha reli, jasiri muongoza njia, shujaa wa Afrika, nuru ya wanyonge,mtetezi wa vijana,simba wa nyika na komandoo wa vita.
Hata angeitwa shetani wa mashetani haiondoi ukweli kwamba huyu ndiye rais kilaza zaidi kuwahi kutokea
 
kama na yeye anatamani sawa lakini kama antaka kujenga legacy asichukue form2025 kwake ni mbali sana ameifungua Nchi lakini hana uwezo wa kudhibiti kila takataka imeingie leo rushwa ni aibu , utoroshaji wa nyala na fedha za nchi umekithili wizi na unyanganyi umeongezeka anakusanya kwenye makapu yanayovuja ingekuwa kheri pale alipofika aridhike na hapo itamjengea heshima sana, hao chawa (vijana) wanaweza wasihimili vishindo vya 2025, nafuu akimwandaa mapema mtu atakaye toka upande wake kuliko kusubili aingie atakaye mtesa yeye na watu wake. na kuifuta historia yake. Mama sisi tunakuombea kama ilivyo wajibu wetu, lakini akili za kupewa ongeza za kwako
 
Rais samia ni mpango wa Mungu mwenyewe na uweza wake Mwenyewe Mungu atamlinda Rais wetu na kumpatia afya njema na nguvu ya kuendelea kututumikia watanzania wote mpaka 2030
Hili taifa likiwa na robo ya vijana wa ajabu aina yako, miaka kumi tu inatosha kuliangamiza. Ni aibu kwa kijana kama wewe kushabikia bila kuangalia changamoto zinazolikabili taifa na aina ya uongozi tulionao. Wewe kutwa kucha ni kusifia tu hata pale panapoitaji kukosoa ili kuonyesha njia.
 
Mimi sisifii Bali naongea ukweli japo ni mchungu kwa baadhi ya watu aina yako.
 
kama na yeye anatamani sawa lakini kama antaka kujenga legacy asichukue form2025 kwake ni mbali sana ameifungua Nchi lakini hana uwezo wa kudhibiti kila takataka imeingie leo rushwa ni aibu , utoroshaji wa nyala na fedha za nchi umekithili wizi na unyanganyi umeongezeka anakusanya kwenye makapu yanayovuja ingekuwa kheri pale alipofika aridhike na hapo itamjengea heshima sana, hao chawa (vijana) wanaweza wasihimili vishindo vya 2025, nafuu akimwandaa mapema mtu atakaye toka upande wake kuliko kusubili aingie atakaye mtesa yeye na watu wake. na kuifuta historia yake. Mama sisi tunakuombea kama ilivyo wajibu wetu, lakini akili za kupewa ongeza za kwako
Acha uongo wako hapa .Rais samia imeiweka nchi katika msitari ulionyooka .nchi ina tabasamu, furaha, matumaini na inapiga hatua za kimaendeleo kwa kasi ya mwanga. Rushwa imedhibitiwa na inaendelea kudhibitiwa kwa yeyote atakayebainika kujihusisha na Vitendo vya rushwa na ufisadi.

Uwezo wa Rais samia kiongozi ni mkubwa sana na ndio maana kwa maono yake makubwa,upeo wake mkubwa ,akili yake kubwa tumeweza kama nchi kujenga uchumi imara unaomgusa kila mtanzania.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika kumekucha,kumepambazuka Tanzania. Bendera imepandishwa,imepandishwa na vijana. Ni bendera ya upendo ,upendo kwa Rais samia kipenzi cha vijana aliyeleta na kuinua matumaini katika mioyo ya vijana,baada ya kutoa maelfu ya ajira kwa vijana serikalini pamoja na ajira mbalimbali zilizotokana na miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa hapa Nchini.

Vijana kwa umoja wao kutoka maeneo mbalimbali nchini wameamua kuchanga hela kwa ajili ya kumchukulia Fomu ya urais mama Samia Mama wa shoka,chuma cha reli, jasiri muongoza njia, shujaa wa Afrika, nuru ya wanyonge,mtetezi wa vijana,simba wa nyika na komandoo wa vita.

Vijana wanafanya haya kuonyesha upendo wao mkubwa kwa Rais samia na namna wanavyomuunga mkono, kumkubali na kuendelea kuhitaji utumishi wake kwa miaka mingine tena. vijana wameguswa na kazi kubwa aliyoifanya Rais samia ndani ya Muda mfupi wa uongozi wake iliyoleta matumaini kwa mamilioni ya vijana.

Hivyo vijana wameona wasikae tu wamebweteka kusubiri kuletewa mgombea ,bali wameamua kuonyesha hisia zao na kupaza sauti zao juu ya uhitaji wao wa kuongozwa na Rais samia kwa muhula mwingine tena. vijana wanataka waweke hatima ya Taifa lao na maisha yao katika mikono Salama ya Rais samia kiongozi msafi, mnyenyekevu, mzalendo, mkalimu, msikivu na mwenye upendo.

Rais samia ndiye chaguo la watanzania, ndiye kiu ya vijana,ndiye aliyeshinda katika mioyo ya vijana.ndio jicho lao lilipotizama kwa matumaini na matarajio makubwa. Hii ndio faida ya kiongozi kugusa maisha ya watu,kuinua maisha ya watu, kuleta matumaini katikati ya kukata Tamaa pamoja na mwanga katikati ya giza.

Lazima watu wakupiganie na wakusemee ni lazima vinywa vyao vilisema na kulitaja jina lako kwa mema,ni lazima watu waziseme sifa zako na kutangaza mema yako. Sasa vijana wanamsemea Rais samia kwa yale makubwa na ya kupendeza aliyoyafanya ndani ya muda mfupi wa uongozi wake yaliyogusa maisha ya mamilioni ya vijana hapa Nchini.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Kumbe ni wewe dubwasha nimesahau nikasoma mavi yako ngoja nikanawe na perfume nyingi!
 
Unaongelea mambo ya 2025 Kama vile unamamlaka ya kujua kitakachotokea. Kikwete alisema mambo yakiharibika Sana Samiah anaweza asigombee.
 
Unaongelea mambo ya 2025 Kama vile unamamlaka ya kujua kitakachotokea. Kikwete alisema mambo yakiharibika Sana Samiah anaweza asigombee.
Taifa lipo salama na linaendelea kusonga mbele kwa kasi ya mshale katika maendeleo.
 
Kikwete hakuongelea vita vya bunduki kaka, kinachoongelewa ni kuchafuka hali ya hewa kisiasa na kutokukubalika kwa Samia, kitu ambacho obviously kinaonekana wazi ndani ya CCM. Huwezi kuona kwasababu wewe ni mgojwa. Hata gogo likipewa urais kwa tabia yako hii ya kujipendekeza na lenyewe utalimwagia sifa.
 
Usisifie mpaka unapitiliza maana unayempa sifa anaweza kudhani unamchora tu! Sasa Samia anakuaje mwamba wa Africa. Samia ameokota tu dodo kwenye mti wa papai basi.
 
Back
Top Bottom