Vijana kwa Wazee:Tuwekeze kwenye miti ya Mitiki

Vijana kwa Wazee:Tuwekeze kwenye miti ya Mitiki

mfano mtiki wa miaka 5 unatumia maji Lita 45 Hadi 60 kwa siku,
Eneo ambalo limepandwa mitiki ukame hushamiri Sana, hivyo mazao mengine huwa hayana uwezo wa kustahimiki hivyo hushindwa kumea vizuri
Upo sahihi kabisa, hilo mimi nimelishuhudia mwenyewe bibi yangu alikuwa anamiti mingi sana ya mitiki huko morogoro kijiji cha Mngeta kama ID yako inavyosoma 😁 mwisho wa siku ardi yote hakuna kinachomea, hadi majirani wakaanza kulalamika, tuliuza yote, ila bei yake ni nzuri.
Kuhusu lifespan yake sina uhakika kama ni miaka mingi sidhan kama inazidi 20
 
Tatizo bado naliona hujazingatia mnyororo wa dhamani kuanzia kulima hadi mlaji.

Kama hawa walaji wa mwisho akitoka kwenye mizunguko yake jioni ananunua mayai mawili, munyu na mafuta kidogo ale yeye na watoto wake alale kisha aamke asubuhi aende kwenye mizunguko yake tena mimi siona mantiki ya kuwekeza huko lazima kufeli tuu.

Sisi twataka tujui soko maana tuliambiw tulime mbaazi, sasa asubuhi ikauzwa 3000 jioni sasa inauzwa 150. Bado kwenye korosho sijazungumzia, bado kahawa, bado mihogo ambayo tunaambiwa unaitajika China, bado kokoa ambayo bei yake ni nzuri baada ya mtekwaji Moo ikabidi ainunue bei nzuri ya shilling 3000 sasa sijui msimu ujao itakuwaje tena...

Za kuambiwa changanya na zako...

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu kama nyinyi wasoma magezeti, makala, vitabu vya uchumi na masoko huwa mnakatisha sana tamaa watu, ndomana wengi wa wasomi mnakufa masikini mnakuja jiimarisha too late na vikokoteo vyenu vya uzeeni. Kila mnachotaka kufanya huwa mnawaza hasara tu. Watu ambao hawana Elimu kama za kwenu wengi huendelea kwa sababu wao huingia field na kufanya na sio kujiuliza maswali kama haya unayoyafikiria.

Wacha uwoga, penda kujaribu.
 
Mleta mada naomba kujadiliana nawe Mambo machache juu ya kilimo Cha mitiki
Kibiashara Ni zao zuri kwani Ni miti yenye Bei nzuri lakini Kimazingira miti hii si rafiki hata kidogo nashangaa Serikali IPO kimya tu hasa kwenye mabonde ya Ulanga, Kilombero na Rufiji
Hakuna tathimini ya Kimazingira EIA iliyotolewa kuonyesha ubaya wa miti hii kwenye mabonde haya, bonde la Kilombero kampuni ya KTC inahadaa na kuendelea na upandaji lkn IPO siku madhara yake yatatugharimu Sana Watanzania hasa kwenye haya mabonde

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
Environmental impact assessment inawezekana imefanyika, sio rahisi kwa project kama hizi kuruhusiwa kirahisi kufanyika katika mabonde hayo ya kilombero, rufiji etc wakati fika wanajua athari zake zitakuwa ni nini, naimani iyo kampuni wala isingepata nguvu hata ya kuhamasisha wadau waje wawekeze kama hivi. na kama kwl serikali imewaruhusu wawekezaji Fanya project kubwa kama hizi bila EIA basi kuna shida mahali
 
Wakati tunasubiri nchi kunyooshwa na
Raisi na kusubiria ntantalila za ccm ... Nawashauri vijana wenzangu na wazee kuwekeza kwenye uwekezaji huu wa mitiki...
Ingieni mtafute maarifa ya huu uwekezaji..!Watu wengi wanafanya hiki kilimo wanapata fedha nyingi..
Maeneo ya kununua mashamba ni mengi.kwa wilaya ya Kilombero na Ulanga...!ardhi kule ipo fertile ..sasa cha kufanya ni ww kwenda na kutafuta ardhi ununue..hapa inategemea na maeneo..na approach yako..lakini hazid laki 3@acre..mbegu na kupimiwa shamba unapata bure kutoka kwa kampuni ya mitiki..!
..Changamoto ni kuisimamia toka unapopanda had 3yrs toka uipande ..!kuanzia hapo haina changamoto sana..
mie maneno mengi sina..tutafute hela jaman..tuwekeze..
miaka mi8 sio mingi kbs kbs ..!

Shime Watanzania! Tukutane2030😊

Nb.Kama upo serious pm me nikupe namba ya mhusika wa KILOMBERO TEAK CO.akupe mwelekeo!
!
Hongera mpapanaji kilimo haki mtupi mtu ukikifanya serious, Mali tutazipatia mashambani. Jaribu hata minazi pia mdau, baada ya miaka 5 utaanza kula wewe utamaliza, watoto watafuata watayaacha mashamba pia, mpaka wajukuu wako wataja nufaika.
 
Bonge ya idea..magereza kun kipindi walokua wanaauza hiyo miche ya muda mfupi..asante sana kwa idea
 
Kwa nini hiyo kampuni ya Teak hawalimi wenyewe kama Sao hill?
Environmental impact assessment inawezekana imefanyika, sio rahisi kwa project kama hizi kuruhusiwa kirahisi kufanyika katika mabonde hayo ya kilombero, rufiji etc wakati fika wanajua athari zake zitakuwa ni nini, naimani iyo kampuni wala isingepata nguvu hata ya kuhamasisha wadau waje wawekeze kama hivi. na kama kwl serikali imewaruhusu wawekezaji Fanya project kubwa kama hizi bila EIA basi kuna shida mahali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonge ya idea..magereza kun kipindi walokua wanaauza hiyo miche ya muda mfupi..asante sana kwa idea
Si limagi mazao ya mda mrefu siku zote, lkn sasa hivi naanza shawishika wkend iliyoisha nilitembelea maeneo ya bagamoyo nilikutana na shule ya nguvu kweli kweli kutoka kwa wakulima hasa wa zao hili la minazi.
 
Upo sahihi kabisa, hilo mimi nimelishuhudia mwenyewe bibi yangu alikuwa anamiti mingi sana ya mitiki huko morogoro kijiji cha Mngeta kama ID yako inavyosoma 😁 mwisho wa siku ardi yote hakuna kinachomea, hadi majirani wakaanza kulalamika, tuliuza yote, ila bei yake ni nzuri.
Kuhusu lifespan yake sina uhakika kama ni miaka mingi sidhan kama inazidi 20

kuna mbegu hybrid..nimeisahau jina lake..bibi aliuzaje
 
Si limagi mazao ya mda mrefu siku zote, lkn sasa hivi naanza shawishika wkend iliyoisha nilitembelea maeneo ya bagamoyo nilikutana na shule ya nguvu kweli kweli kutoka kwa wakulima hasa wa zao hili la minazi.

huo ni uwekezaji...ukifumba macho kwakweli lazima uje ushangilie..!huko bgmy wana hyo mbeg ya muda mfupi?all the best
 
Oky, kila la kheri mkuu

Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau

Wewe msomi wa Mngeta unatokea maeneo gani pale? Lukolongo, Mkangawalo, kotako au Mchombe?
Hilo bonde la Kilombero kuanzia Kidatu, Msolwa, Sanje, Mkula, Sonjo, Mang'ula,Kisawasawa, Kiberege,Signal, Ifakara, Idete, Namwawala, Mbingu, Mngeta, Ikule, Chita, Udagaji, Chisano hadi Mlimba nilishapita sana miaka ile nilipokua nafanya biashara ya kununua mchele.

Achilia mbali upande wa Mahenge na Malinyi.
 
Kama unataka kufa kwa Stress wekeza kwenye hiyo miti. Inachukua miaka 60 kupata mavuno. Hivyo usiiwekeee maaanani ya miaka 10 au 20 ni UONGO. Soft woods kule Mufindi sawa lkn hizo Hard Woood! Usitafutie watu umaskini na Stroke bureee
Alichosema mtoa mada ni sahihi, mambo yamebadilika. Zamani mpunga na mahindi ilikua miezi 6, sasa ni miezi 3 tu. Hata Mitiki ipo ya kisasa ya kuanzia miaka 8 inavunwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati tunasubiri nchi kunyooshwa na
Raisi na kusubiria ntantalila za CCM.

Nawashauri vijana wenzangu na wazee kuwekeza kwenye uwekezaji huu wa mitiki.

Ingieni mtafute maarifa ya huu uwekezaji..!Watu wengi wanafanya hiki kilimo wanapata fedha nyingi.

Maeneo ya kununua mashamba ni mengi.kwa wilaya ya Kilombero na Ulanga...!ardhi kule ipo fertile

sasa cha kufanya ni ww kwenda na kutafuta ardhi ununue hapa inategemea na maeneo na approach yako lakini hazid laki 3@acre mbegu na kupimiwa shamba unapata bure kutoka kwa kampuni ya mitiki..!

..Changamoto ni kuisimamia toka unapopanda had 3yrs toka uipande ..!kuanzia hapo haina changamoto sana..
mie maneno mengi sina..tutafute hela jaman..tuwekeze..
miaka mi8 sio mingi kbs kbs ..!

Shime Watanzania! Tukutane2030[emoji4]

Nb.Kama upo serious pm me nikupe namba ya mhusika wa KILOMBERO TEAK CO.akupe mwelekeo!
Naona siasa zinakunyanganya ndugu. Huyo alikuongopea atakuua kwa presha. Hiyo miti inachukua miaka mingi sana na siyo nane kama unavyotaka kuaminisha
 
Kama unataka kufa kwa Stress wekeza kwenye hiyo miti. Inachukua miaka 60 kupata mavuno. Hivyo usiiwekeee maaanani ya miaka 10 au 20 ni UONGO. Soft woods kule Mufindi sawa lkn hizo Hard Woood! Usitafutie watu umaskini na Stroke bureee
Ila mitiki in issue kukua mm ninamtiki 1 hapa mwanza s unamiaka 20 lakini bado unahitaji miaka mingine kama 20 ili uweze kuvunwa
 
Back
Top Bottom