Vijana, kwanini hamuwatunzi wazee wenu?

Vijana, kwanini hamuwatunzi wazee wenu?

Nyie vijana acheni tabia yakuwakana na kutowatunza watoto pale mnapowazaa...tabia hiyo inawafanya mkifikia uzeeni muanze kuwalaumu watoto wenu....andaeni uzee wenu vizuri watoto wawe ndio hazina yenu ya kesho
Inatakiwa mtu akishafikisha miaka 45+ aanze kujipanga kwa uzeeni, kama kuna watoto kila kona, aangalie namna ya kuwapa haki zao za msingi
 
Na wale wazee waliotelekeza familia zao, watoto wakapambana kivyao au kwa support ya watu wengine hadi wakatoboa(wakawa na uhakika wa milo 3 kwa siku). Hawa wazee pia tunawazungumziaje?
Baba ni baba as long as wewe ni damu yake.

Baba ndo anatoa baraka.

Wanawake wamevamia ukweli wanataka wao waonekane ndo wafungua njia

Lakini Biblia inasema baba ndo mwenye ufunguo wa baraka zako
 
Kama huna shida yoyote, kati ya 21 mpaka 24 una mtoto, 27 una mtoto, 33 mwisho wa kuweka mtoto. Ifikapo 60, uliyempata ukiwa na 33 anakuwa na 27, kama hajiwezi pumbavu zake, asikujue, uzee ni wako, pension ni yako!
[emoji38][emoji38][emoji38]
"Kama hajiwezi pumbavu zake, asikujue"
Huu ni ukweli mchungu.
 
Baba ni baba as long as wewe ni damu yake.

Baba ndo anatoa baraka.

Wanawake wamevamia ukweli wanataka wao waonekane ndo wafungua njia

Lakini Biblia inasema baba ndo mwenye ufunguo wa baraka zako
Kama hakutoa matunzo inakuwaje?
 
Siyo hao tuu Mzee yeyote yule .. ajilee yeye mwenyewe .

Wewe na mimi (watoto wetu tulee familia zetu)
Kiufupi, wazee wanapaswa kuwatengenezea watoto wao mazingira ya wao kuja kulelewa baadae.

Kama baba ingali ana nguvu, hakujali familia asitarajie aje apendwe baadae na kulelewa.

Hivi mzazi akiisuka familia yake ipasavyo tangu ikiwa changa, akalea vizuri, akawatengenezea mazingira ya kutoboa, unadhani hapo arasahaulika baadae, hapana.

Chanzo kikubwa cha wazee kutelekezwa na watoto wao ni wao kutowajali na kuwajengea misingi ya kutusua(japo kuwaweza kupata elimu) ingali wakiwa wanahitaji msaada wa mzazi.
 
Baba ni baba as long as wewe ni damu yake.

Baba ndo anatoa baraka.

Wanawake wamevamia ukweli wanataka wao waonekane ndo wafungua njia

Lakini Biblia inasema baba ndo mwenye ufunguo wa baraka zako
Wengine tumekulia mikononi mwa ndugu wengine katika ukoo utadhani ni mayatima kumbe sio hivyo ila sababu mzee ni chenga(tena anajua ila kujifanya nunda na misimamo ya kikoloni).

Wazee wa hivi wanatia hasira sana
 
Hilo ndilo shamba la mibaraka sasa. Ukimsaidia mzee wa hivi utabarikiwa mpaka ushangae. Hata kama una kinyongo naye bado msaidie ukiwa mbali...fanya hivyo utakuja kuniambia. You raise above the fray labda awe pasua kichwa kama huyu wa Dimples nimemuona anatema nyongo kwenye tivi nikasema huyu mzee ni zero na hajajifunza cho chote...
 
Matunzo(kulea kwa nyanja zote muhimu) ndio Amali njema ya wazee kukumbukwa.
Tatizo linaweza kuanzia kwenye mahusiano yao, labda hayakuwa mazuri,ikafikia kutelekeza mtoto
 
Back
Top Bottom