Siku zote huwa nawaambia vijana fanyeni siasa, fanyeni ushabiki wa kisiasa, wapendeni viongozi wa kisiasa lakini kamwe msije kujitoa mhanga kiasi kwamba mnahatarisha maisha yenu kuwapigania wanasiasa au vyama vyao.
Wanasiasa wote unaowajua wapo pale kwaajili ya maslahi yao na familia zao kwanza na ndio maana unaona sio rahisi kuachia madaraka kirahisi. Kuna maslahi makubwa sana kwenye hivi vyama vikubwa mfano CHADEMA.
Kuna pesa nyingi inayoingizwa kwenye chama inayoonekana na isiyoonekana na nyingi hazikaguliwi na wala hazijulikani hata na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG). Mfano kuna pesa inatoka kwa watu binafsi ( matajiri ambao wanasapoti upinzani lakini hawataki kujulikana), pesa kutoka kwa Diaspora, wafadhili wa nje, vyama rafiki n.k, ukiachana na Ruzuku za serikali na ushawishi kutoka serikalini kupitia ishu kama za maridhiano.
Lakini pia nafasi za uongozi mfano wa viti maalumu huwezi kupata kama huna connection na viongozi wa juu...Ndio maana karibu nusu ya COVID 19 ni wake za vigogo CHADEMA.
Na kama unataka kuamini bongo hakuna upinzani bali ni maslahi ya wachache, angalia kipindi cha Magufuli wale wabunge na madiwani wa upinzani hasa CHADEMA wewe uliokuwa unawaamini sana na ulijitoa sana na kuwatetea sana, walivyoshawishiwa na kununuliwa kirahisi tu kwa ahadi ya vyeo!
CCM itaendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingi sana ijayo endapo hakutatokea chama na viongozi wenye nia ya kweli ya kuikombia nchi hii.