Vijana msio na ajira jikusanyeni mchukue nchi 2030

Kwanza unazungumzia vijana wapi? hawa hawa wa Simba na Yanga au?
 
Tunawapa mikopo rafiki? Tumewaandalia mazingira mazuri ya kilimo?

Ndiyo maana wanakiogopa kilimo.... wakimbilie mashambani wakalime mchicha unaonunuliwa sokoni mitano!!!
Serikali sikuvu ya CCM chini ya kiongozi mkuu na kipenzi cha waTanzania wote Dr.Samia Suluhu Hassan ameliunganisha na kuifungua nchi na kua na mazingira bora zaid ya kiuchumi, kisiasa na kijamii,

Ndio maana Tanazania ndio nchi pekee kwenye kanda ya maziwa makuu yenye mazingira bora na mazuri zaidi kibiashara, kilimo, ufugaji, usafishaji n.k

Hata hivyo,
kua tajiri au maskini Tanzania ni uamuzi binafsi wa mtu,
Na uvivu na uoga wako ndio chanzo cha umaskini wako πŸ’
 
Watu wanazungumzia kilimo kama kitu cha kawaida kama huna mtaji kilimo cha kupiga jembe kwa mkono ni kigumu na kinazeesha sana
 
Nimekuelewa saana tu.

Nguvu kazi bado ni tatizo.... hapa nitatofautiana na wewe. Nguvu kazi bado ni tatizo tena ndiyo imekuwa tatizo haswa maana kwasasa tunahitaji well trained, sophisticated and highly skilled human resource.

Hatuna uhitaji wa kuangalia nini kifanyike maana waliopaswa kuangalia wameshindwa. Vijana waingie mzigoni vijana wa wazee waliopo madarakani sasa nao wataabike ili tuongee lugha moja.

Hauwezi kutafutiwa suluhisho na mtu ambaye tayari anajua mwanae atafanya kazi BOT akimaliza chuo, nephew atampeleka States kufanya MBA kisha akimaliza anampeleka TANAPA, ......
 
Mazingira gani..... labda anajaribu ila kasi ya mabadiliko haiendani na kujaribu kwake.

Fuatilia historia ya makampuni makubwa kama Toyota, Honda serikali iliyagroom.... wachina wanapewa mikopo Kuja kuchuuza Africa.
 
Watu wanazungumzia kilimo kama kitu cha kawaida kama huna mtaji kilimo cha kupiga jembe kwa mkono ni kigumu na kinazeesha sana
Hawa ni watoto wa kishua.

Kama unataka vijana waingie kwenye kilimo waki-pimp kwanza...wakiwekee rims na sound system.

-Soko liwe la uhakika
-mikopo iwe sawa na Bure
-wajenge viwanda vya uchakataji tusiuze ajira nje.
N.k
 
Na ndiyo majibu yao hawa wazee waliotoboa kupitia kodi
Tafuta kazi ya kufanya hamna mtu atakaekubali kufa Kwa ajili Yako nchi hii kiufupi tanzania unatakiwa ku mind your business
 
Nimekuelewa saana tu.
Wewe unaongelea kubadilishana yaani hii Keki chache kwamba ifike wakati na nyie wachache mpate hio keki na sio kuangalia ufumbuzi wa kuongezea Keki ili watu wote wapate (na sio kesho bali leo) sababu kubalisha watu na sio system itakuwa ni yaleyale (chupa tofauti mvinyo uleule)
Nguvu kazi bado ni tatizo.... hapa nitatofautiana na wewe. Nguvu kazi bado ni tatizo tena ndiyo imekuwa tatizo haswa maana kwasasa tunahitaji well trained, sophisticated and highly skilled human resource.
Nope tunapoelekea uhitaji wa nguvu kazi haupo tena; hapo kale watu waliajiri watu ili wahesabu pesa, zikaja money counter na sasa hivi ni digitally wala huitaji kushika noti..., kuna kipindi mtu anakwenda dukani kununua vitu leo hii online hata kama kitu kipo Amazon warehouse huko Ughaibuni kinakufikia; nikiuza kitu point of sale inafanya accounting zote sihitahi muhasibu; nikumwa nikiweka details za ugonjwa wangu napewa mkeka ya huenda naumwa nini..., Zamani watu mia wangelima na kupata gunia mbili leo hii combined harvester linafanya kazi usiku na mchana na mkulima mmoja anaweza kulisha nchi nzima...
Hatuna uhitaji wa kuangalia nini kifanyike maana waliopaswa kuangalia wameshindwa. Vijana waingie mzigoni vijana wa wazee waliopo madarakani sasa nao wataabike ili tuongee lugha moja.
Kwahio sio kwamba unatatua tatizo unabadilisha wataoa matatizo ? Ndio maana nimekwambia uhitaji kusubiri inabidi ushinikize kuanzia leo..., ila kitakachotokea kwa sisi tunaofuatilia historia hapo keshokutwa kama dunia haitabadilika yatatokea ya French Revolution na watu kupigana..., Absolute Poverty anywhere is a threat to Society Everywhere...
Hauwezi kutafutiwa suluhisho na mtu ambaye tayari anajua mwanae atafanya kazi BOT akimaliza chuo, nephew atampeleka States kufanya MBA kisha akimaliza anampeleka TANAPA, ......
Again unaangalia kwa jicho la wachache (Individually) mimi naongelea collectively na ukweli ni kwamba middle class inazidi kupotea na kuna ongezeko la wachache sana ambao wanakula na kusaza na majority hawana hata makombo..., And that my-friend, is a recipe for disaster.
 
Hehe! viongozi wakipewa hela tu kwisha chama cha vijana wasio na ajira!..
heri vijana hao waongee na chama kimoja wapo cha upinzani waweke makubaliano kuwa wao wanahitaji hiki na hiki, halafu wenyewe wakipe hicho chama sapoti ya kura kwenye kushika nchi!.
 
Mazingira gani..... labda anajaribu ila kasi ya mabadiliko haiendani na kujaribu kwake.

Fuatilia historia ya makampuni makubwa kama Toyota, Honda serikali iliyagroom.... wachina wanapewa mikopo Kuja kuchuuza Africa.
mazingira ya kilimo ni bora na mazuri sana, mazingira ya ufugaji, uwekezaji, biashara na usafishaji ni mazuri zaidi, amani, ulinzi na usalama ni vya kuaminika mno n.k

mtu mvivu na mzembe hawezi kamwe kuyaona haya gentleman πŸ’
 
kwenye nafasi ya uraisi waniachie
 
Haiwezekani...
Kayavamie ulime uone moto wake wanakuja kufyeka yote na kukufukuza kwamba sio mali yako mbwa wewe hii mali ya Serikali unalima pori la kwako hili? Wewe kibwengu haujui unabwatuka tu kuna mapori mapori ya baba yako yale? Kayaguse uone cha moto
 
mazingira ya kilimo ni bora na mazuri sana, mazingira ya ufugaji, uwekezaji, biashara na usafishaji ni mazuri zaidi, amani, ulinzi na usalama ni vya kuaminika mno n.k

mtu mvivu na mzembe hawezi kamwe kuyaona haya gentleman πŸ’
Wewe kibwengu wa CCM tulia hapa watu wanajadili mada serious utani wako wa kawapelekee vibwengu wenzio kule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…