Nimewahi Kuandika Humu, Siku za nyuma kama sio 2017 basi ni 2018 ama 2019, Mchepuko alituma msg, na Mama alikua ameniandikia Naomba Nipigie, Nikasema wacha Nimjibu mchepuko kisha mama Nitampigia.
Kilichotokea Msg ya Mchepuko ikaenda kwa mama, halafu Nikampigia kama nilivyopanga, Tukazungumza Vizuri kabisa wala hakuuliza kitu nami sikua nimefahamu kama nimekosea.
Baada ya masaa kadhaa kupita mchepuko akanipigia akilalamikq Sijamjibu msg yake, Nikamwambia nimekujibu ngoja nicheki huenda ili fail. Kucheki Lahaula nakuta mzigo mzima umeenda kwa mama [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] nikasema sasa hapa nakausha siombi hata msamaha, By the way yeye si mama yangu [emoji3][emoji3].
Ilipofika jioni mama akanijibu ile msg kwamba " Mwanangu mimi sio babe wako, Na kuwa makini usimuumize mkeo na jihadhari na magonjwa" Aiseh nikasema hapa simtafuti tena mama [emoji3][emoji3]
Kesho yake mchana akanipigia simu anauliza ujumbe wake niliuona???
Nikamwambia mama hizi simu Zitakuja kugombanisha watu [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] akacheka tu akasisitiza niwe makini na ujumbe wake niuzingatie.