Ni ukweli bila chenga kuwa uuguzi kote duniani ulichelewa sana kupata wahitimu wenye degree, masters na PhD. Uuguzi ulikuwa kazi ya maelekezo Tu. Udaktari Kwa muda mrefu sana ulichukua vijana werevu wenye matokeo mazuri darasani. Hivyo tangu zamani walikuwa na maprofesa wengi na watu wengi waliosoma, Makerere, Uingereza, urusi, Israel, ujerumani, Italy na mwingine kwingi. Hii iliwafanya DK wawe juu kwenye sectors za afya kwakuwa no kweli kabisa walikuwa na elimu na exposure kubwa kuliko wauguzi ambao wengi wao walikuwa darasa la Saba na form IV failure. Hii ilisababisha hata viongozi wa wengi wa uuguzi kwenye ngazi zote wawe inferior mbele ya wenzao wa udaktari. Mbaya zaidi madaktari wengi walioa manesi, hii nayo ilizidi manesi wawaheshimu madk kama senior lakini kama waume na shemeji zao pia.
Hali hii ilisababisha vijana wenye elimu ya sayansi wengi wajiunge na udk na wauone udk ulikuwa mzuri kuliko uuguzi. Kwasababu ya elimu kubwa hata kipato chao pia kilikuwa kikubwa kuliko kile cha wauguzi wasio na elimu, TNs.
Mambo sasa ni tofauti, nyumbani kumenoga. Nurses sasa wanakijua kile wanachokifanya. Wanasoma na baadhi ya vile kilikuwa vinasomwa na MD tu.
Baada ya kila mtoto na mzazi kutaka mtoto wake awe DK, sasa hivi vijana hao wamekuwa wengi mnooo kuliko mahitaji (saturated) baada ya vyuo vingi kufunguliwa na kuzalisha madk wengi.
Baada ya huduma za jamii kuboreka, kuenea kwa preventive health services na elimu ya afya kuenea hivyo kusababisha magonjwa na wagonjwa kupungua kwenye jamii, nafasi ya udaktari inazidi kuwa finyu, hakuna malaria, cholera, tz, and others unhygienic diseases nyingi siku hizi duniani kote why more dks? Kunahitajika wachache Tu wenye ujuzi mkubwa kwaajili ya emergencies, na chronic non communicable diseases wengi.
Hata hapa nchini vijana walimaliza MD wakatagutiwa nafasi za waliogoma huko Kenya.
Kinyume chake Wauguzi wanahitajika wengi Sana wodini, kwenye research, mashuleni, viwandani, migodini, bandarini, jeshini, nyumba za wazee, labor ward, family planning, kwenye chanjo, Kwa wakimbizi, kwenye kufundishia vyuoni, kwenye uongozi, kwenye uwandishi wa vitabu, na kwenye clinic na outreach mbalombali. Nurses pia kama wengine wanaweza kuendesha maternity home care zao na kufanya biashara na kilimo kama wakitaka maana hawaendi kwenye viosk vya wahindi mchana kutwa kama kaka zao madk ambao usiku kucha na vimanati vyao shingoni, no time to rest or even think. Kila wakati wanaongelea hadithi za wodini, wagonjwa na ccd hata kwenye grocery za pombe, huruma hawana kingine wanafahamu na wanasimulia isipokiwa wagonjwa hata kwenye mazishi.