tuweke pembeni biashara, tuzungumze uwekezaji.
Tafsiri rahisi ya huku Uswahilini, Uwekezaji ni kitendo cha kufanya jambo litakalo kuja kukufaa baadae, huku ukivumilia na kujizuia sana ili ufikie utakacho. Ndo maana kuna watu waliwekeza kwenye elimu nzuri kwa watoto wao, bila kujali kama wanaweza kufa. Wengine wakanunua mifugo, wengine wakapitia kila bar iliyofunguliwa. hizi za kununua hisa ni ktk ulimwengu wa kisasa, zamani pia watu waliwekeza ktk namna ya ulimwengu ulivyokuwa, mfano; kufanya matendo mema kwa jamii, nao ni uwekezaji kwa miaka ile, pengine hata leo. Kumcha Mungu ni uwekezaji pia.