Vijana tuongee kuhusu fursa mbalimbali ikiwemo biashara

Vijana tuongee kuhusu fursa mbalimbali ikiwemo biashara

Ukipewa mtaji uaminike kijana

M nafuga kuku zenji na kilimo cha pilipili mwendokasi anotaka kunipa soko karibuuu
Tataizo vijana ukiwapa mtaji wanapotea uaminifu sifuri ndio shida
 
Kuna mchongo nimeupambania ndani ya mwezi huu natarajia kupata kama milioni 4 hivi. Makazi yangu ni dar na iringa. Hapa nafikiri niingie kwenye mishe za kuuza jezi dar lakini nawaza iyo biashara ni ya msimu, ikifika november tu watu washanunua jezi za timu zao pendwa hakuna biashara tena. Nikifikiria niweke kituo iringa niingie kwenye mishe za kuuza mbao napo naona mtaji hautoshi. Kati ya iringa au dar nikipata location nzuri ya kufungua car wash najitosa humo humo.
 
Tataizo vijana ukiwapa mtaji wanapotea uaminifu sifuri ndio shida
Mtu hana ujuzi wala uzoefu wa biashara yoyote halafu unampa mtaji unategemea nini. Mshirikishe kwenye michongo yako akishaiva mpe mtaji akajisimamie mwenyewe.
 
Kuna mchongo nimeupambania ndani ya mwezi huu natarajia kupata kama milioni 4 hivi. Makazi yangu ni dar na iringa. Hapa nafikiri niingie kwenye mishe za kuuza jezi dar lakini nawaza iyo biashara ni ya msimu, ikifika november tu watu washanunua jezi za timu zao pendwa hakuna biashara tena. Nikifikiria niweke kituo iringa niingie kwenye mishe za kuuza mbao napo naona mtaji hautoshi. Kati ya iringa au dar nikipata location nzuri ya kufungua car wash najitosa humo humo.
Car wash ukipata eneo zuri inakutoa.
 
Wakazi wa iringa mjini mliopo humu tupeane mawazo ya fursa za biashara. Nimekaa takribani miaka miwili iringa mjini nimeona kuna trend kubwa ya kufungua car wash pembezoni mwa biashara. Pia mikopo ya wasiliamali aka kausha damu kuna viofisi kila mtaa lakini sijafanya uchunguzi kama izo mishe zinalipa. Kwa maono yangu iringa ukiwekeza kwenye biashara ya pombe utapiga hela maana kule asubuhi tu watu wapo kirabuni au kwenye vigrocery wanakunywa halafu sasa wanawake, wanaume, mpaka mabinti wadogo kabisa wote walevi. Sema hasara yake kuna ukabira sana wateja wana-prefer zaidi kununua kwa wahehe wenzao. Mchongo mwingine niliouon iringa ni kwenye usambazaji wa mafuta ya vyombo vya moto sheli zipo mbali mbali sana ukisogea pembezoni ya mjini kidogo ukaweka kituo cha kishkaji tu cha kuuza mafuta unapata wateja.
 
Mtu hana ujuzi wala uzoefu wa biashara yoyote halafu unampa mtaji unategemea nini. Mshirikishe kwenye michongo yako akishaiva mpe mtaji akajisimamie mwenyewe.
Sasa jamani ujuzi wa bodaboda nao mpaka tushirikishane kwanza
 
Back
Top Bottom