Wakusoma 12
JF-Expert Member
- Jul 3, 2017
- 5,503
- 15,858
Wakuu, nimeona niweke hili wazi kabisa kwa sababu mambo yanayojitokeza mitandaoni na mtaani si ya kubeza.
1. Kila mtu anapenda kuona mabadiliko na maendeleo, lakini hakuna kinachojengwa kwenye vurugu. Historia imeonyesha mara zote: fujo zikianza, wa kwanza kuumia ni vijana wenyewe.
2. Tumegeuzwa “remote control” za watu ambao hata hawapo ground. Wao wanalala usingizi mzuri, sisi ndiyo tunabeba madhara, kesi, majeraha na kukosa fursa. Tukatae kutumika kirahisi hivi.
3. Amani haimaanishi kukubali kila kitu kimya kimya, hapana. Inamaanisha tunapigania haki kwa njia za busara, hoja, na mazungumzo, si kwa kutishiana wala kuvuruga watu wengine.
4. Vijana wengi leo wanahangaika na ajira, elimu, biashara, mashamba na familia. Ukishabikia fujo, kesho mambo yakienda mrama, ni wewe na maisha yako vinavunjika. Hakuna sponsor wa vurugu atakayekulipia hasara yako.
5. Jambo lolote linapofika hatua ya maridhiano, Serikali na wasemaji wake wanasema wapo tayari kusikiliza—basi na sisi vijana tuwe sehemu ya suluhu, si sehemu ya visingizio vya kuharibu utulivu wa nchi.
6. Tuwe na msimamo mmoja:
Hakuna kupambana kwa fujo. Tunapambana kwa hoja, kwa heshima, na kwa kusukuma mazungumzo yenye tija kwa taifa.
7. Vijana tukae tukijua: Amani ni mtaji. Bila amani hakuna uwekezaji, hakuna mikopo, hakuna biashara, hakuna ajira. Yote haya yanatuhusu sisi moja kwa moja.
8. Kwa kifupi:
Tusikubali kushabikia uvunjifu wa amani.
Tuwe watulivu, wenye busara, na wazalendo wa kweli.