Vijana tuwe makini: Uric acid, UTI sugu, blood pressure, anthritis, KDC, brusella na kisukari kuokota rahisi sasa hivi!

Vijana tuwe makini: Uric acid, UTI sugu, blood pressure, anthritis, KDC, brusella na kisukari kuokota rahisi sasa hivi!

■Tuache vitu vitamu sana kama soda na carbonated drinks

■Tupunguze nyama nyingi nyekundu

■Tupunguze beer

■Tuache sex za kavu kavu

■Tupunguze mafuta mengi katika milo e.g vyakula vya kukaaga na mafuta mengi

■Tujifunze kunywa maji. Hapa ndio kuna uvivu ila hauna namna itakubidi tu

■Tupunguze sukari nyingi.

■Tuache kukaa muda mrefu kwenye viti vigumu na vilivyonyooka e.g gharamika ununue viti maalum

■Tupunguze uzito.

■Tupunguze kunywa maziwa sana


Miaka tu 20 iliopita usingeweza kuona tabu hizi lakini sasa hivi zimekuwa chronic katika jamii, na sasa cha ajabu mostly katika vijana wadogo mno.

Najua hata wewe hapo haukosi ndugu au rafiki wa karibu ambae hakosi moja ya hizo conditions hapo juu.

Tumejitahidi kiasi kushindana na ukimwi, sasa hivi tushindanae na haya majanga mengine.

Mzungu cancer ndio inampa tabu, Waafrika tabu zilizo kuja ni hayo majanga niliyotaja hapo juu. Yana tesa sana, yana gharamisha na pia kifo cha uchungu sana.

Kama ni vigumu kufanya mazoezi jichange ununue kabaiskeli ka mazoezi weka ndani uwe unapiga mazoezi asubuhi na jioni.

TAKE CARE. Hamka sasa Kafanye full check up ya mwili mzima na full blood picture ili ujue status zako ili upambane na viatirishi vitakavyoonekana katika mwili wako
We umetaja majanga au umetaja risk factors? ilifaa baada ya hapo uoneshe na yatokanayo kutokana na hizo risk factors kwa kupambanua kwa mujibu wa title ya uzi wako mkuu kwa faida ya wengi wasiojua. Na ningeshauri pia utenganisha yanayoambukizwa na yasiyoyoambukizwa maana nadhani week hii tuna kongamanao la kupambana na hayo magonjwa yasiyoambukizwa kuna watu bado tunaamini kisukari na pressure ni magonjwa ya kuambukizwa na sio kutokana na tabia au mfumo wa maisha. Asante kwa uzi adhimu ila kuna vitu ambavyo ni vigumu kuviacha hasa kwa sisi vijana. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo sasa kwa miaka hii kati ya watu wa tatu wenye umri wa kati (vijana) mmoja ana tatizo mojawapo ya uliyotaja hapo juu tofauti na miaka ya 80 ambapo ni mtu mmoja kati ya watu kumi, na kimsingi kwa sasa kila familia au kaya ina victim mmoja.

Zamani wanywa beer wakubwa walikua wazee ila kwa sasa utitiri wa sehemu za starehe vijana tunaongoza kwa kukesha baar na kupanda juu ya meza hali inayosababisha over-consumption ya alcohol na kuamka asubuhi tukisifu kwa idadi ya beer na nyama tulizokula na matokeo yatokanayo ikiwemo ngono. NAAMINI WEWE NI MTAALAMU KAA UANDIKE UZI MUJARABU KWA FAIDA YETU NA KIZAZI CHETU
 
Labda uwe maskini wa kupindukia
Ila ulivyotaja ndio inasukuma mwanadamu kutafuta maisha kwa nguvu zote

Haha 😆

Watakusikia kaka ambao wanataka kuishi milele

Ongeza na wasipande Bodaboda maana ni zaidi ya hivyo
Hakikisha ukiumwa haufilisi watu. Siyo unasema hivi kwa kiburi halafu ukiumwa unaenda kwa wazazi kusumbua na kuomba michango ya ndugu.
 
Usinywe bia, usinywe maziwa, usile nyama nyekundu.

Wazee wetu wamekula nyama, wamekunywa maziwa, wanakunywa pombe tena za kienyeji, wamevuta kiko.

Kuna kitu hakipo sawa.
 
solution ni kufanya mazoezi na kumuomba Mungu akuepushie mbali na maradhi
Wengi wamekufa kwenye mazoezi sababu ya kutoanza kwanza kwa daktari au wataalamu wa afya kujua ni aina gani ya mazoezi wanayotakiwa kufanya na kwa kiwango kulingana na hali za kiafya za miili yao. Ushauri ni kwamba lazima kumona Daktari kwanza na kufanya vipimo stahiki vya mwili (check up) kabla ya kuingia kwenye mazoezi.
 
Labda uwe maskini wa kupindukia
Ila ulivyotaja ndio inasukuma mwanadamu kutafuta maisha kwa nguvu zote

Haha 😆

Watakusikia kaka ambao wanataka kuishi milele

Ongeza na wasipande Bodaboda maana ni zaidi ya hivyo
Kuna jamaa mmoja alienda kufanya major medical chechup kwa specialist na baadaye dakta alipomwita ili ampe matokeo mazunguzumzo yalikuwa hivi:
Dakta: Majibu yanaonyesha kwamba kwa umri wako wa miaka hamsini, una afya nzuri kabisa, hakuna tatizo.
Jamaa: Asante dakta, unadhani ninaweza kuishi kufikisha miaka 85 au zaidi?
Dakta: Unakunywa pombe?
Jamaa: Sionji hata tone na sijawahi kabisa.
Dakta: Unakula nyama au vyakula vyenye mafuta kwa wingi?
Jamaa: Hapana, hivi vitu natumia kwa nadra sana.
Dakta: Mambo ya kujirusha na wanawake je?
Jamaa: Huko nako siko kabisa, mimi muda mwingi nautumia kwenye kufanya mazoezi
Dakta: Sasa kama vyote hivyo hutumii, unataka kuishi miaka 85 ya nini?
 
Back
Top Bottom