DolphinT
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 2,014
- 2,979
Naam hilo ni muhimu sana, kwa sbabu kila chakula kinahitajika mwilini kwa kaisi chake ndio maana kuna balanced diet au mlo kamili. Kuacha aina flani ya vyakula kwa kudhani kwamba vinaleta athari za magonjwa kwenye mwili ni kutengeneza tatizo jingine ambalo ni kubwa kuliko unalojitahidi kuzuia. Kwanini kula nyama choma na bia kila siku? tena kwa kiwango kikubwa? kula mlo kamili kwa kuzingatia uwiano hii itasaidia kubalance na kuupa mwili nafasi ya kuchakata na kutoa kile ambacho hakihitajiki kwa mifumo yake. Mfano mtu ambaye anakunywa beer 20 kwa kikao kimoja kila siku jioni, kitimoto, na aweke KVANT Ndogo au nyagi kuboost, halafu asubuhi aamke na mning'inio apige soup na chapati mbili aende ofisini akae kwenye key board na kiyoyozi kama mimi hawezi kuwa sawa kiafya kama mtu anayekunywa bia nne wikend na nyama siku ya jumapili tu"Kwa hiyo kampeni tunayopaswa kuihimiza ni ubora wa chakula sio kuacha kula.
baadae tunajidanganya Tajiri akila dagaa ni diet ila maskini akila dagaa ni njaa, na tajiri akitembea ni mazoezi na maskini akitembea hyana nauli. we need to habe a comprehensive change of mindset behaviour and habit kwa ujumla katika kila nyanja ikiwemo kuwajali wenzetu. How comes unawapa kuku dawa za binadamu? how comes unachoma mnyama sindano leo halafu kesho unamchinja? how comes unampa nguruwe ARVS? How comes unapiga mboga mboga viwatilifu halafu baada ya siku mbili unavuna kisa umepewa tenda ya ghafla?