View attachment 2707633
Kunahitajika PROGRAMU ya dharura kuliokoa hili jiji.
Vijana wengi ni waliozaliwa na kukulia hapa hapa ni jamii za wazawa wenye asili ya Arusha kama Wameru na Waarusha pamoja na jamii za wenyeji ambao walihamia na wapo kwa muda mrefu kama Warangi, Wachaga, Wambulu, Wnyaturu.
jamii za mikoa ya karibu waliohamia Arusha kwa muda mrefu (sio wakuja). hapa wapo Wameru, Waarusha, Warangi, Wachaga, Wambulu, Wanyaturu.
matokeo ya kuukuta utamaduni wa kutukuza uhuni tangu wakiwa wadogo, imeshakuwa ndani ya mfumo wa maisha wa vijana wengi kwamba ili uonekane mjanja basi uwe mhuni wa kunywa pombe kali, kuvuta bangi ama uwe mhalifu.
mapikipiki haya ya wanakimbiza vibaya mno, ajali kila siku, wamejaa mount Meru na nkoaranga hospital wamevunjika vunjika miguu,.Bodaboda za kutaftia riziki wanalazimisha ziwe pikipiki za michezo, ukienda kwenye magroup yao haya ya kudandia pikipiki kuna "pumzika kwa amani / rip" nyingi sana.
vijana wanazidi kuutukuza ulevi wa hayo ma k-vant na bangi, sina shida na matumizi ya vilevi hata mimi ni mdau ila nafata misingi,tatizo ni pale wanatumia vilevi kupita kiasi na ku abuse (abnormal use), wanatumia kwa kuigana au ile kutaka kuonekana mzoefu ili kupata sifa za kuonekana ni moja wao, na ndio hapa mtu ananasa kwenye uraibu.
Makundi ya vijana wengi ni magenge ya vijana wanaoishi bila future, wanafanya vingi bila kujali madhara wala kesho.
Suala la kupigana beto (visu) nalo halipo nyuma, Sime na visu vimekuwa vitu ambavyo vinazidi kuzoeleka kutumika sio tu kwenye uporaji bali hata kwenye mabifu ama ugomvi baina ya vijana, niliwahi shuhudia live kwa macho yangu pale karibu na stendi ugomvi niliodhani watu watachapana ngumi niliona mtu anapigwa kisu damu nje nje,kuna clip nimecheki majuzi Fidovato analalamika vijana wanapigana beto, hata wasanii wa huko Father Nelly wa kundi la X Plastaz aliuliwa kwa visu, nae Lord Eyes aliwahi kujeruhiwa,
Wizi nao hauna dalili ya kupungua, watu wanaporwa kikatili sana inabidi utii amri lasivyo utavurugwa maini na beto, bodaboda wanaibiwa pikipiki mpaka kuuwawa, ujambazi nao upo wa kuvamia matajiri, kwa ufupi kuna famjlia zinajulikana kabisa wanaishi mjini kwa shughuli hizo lakini ndio wanapewa heshima maana uhuni unaonekana ujanja.
Ajabu ni kwamba hata polisi ni kama vile wamefumbia jicho ama jitihada wanazofanya ni ndogo sana, ni kama vile wamezila na kujikatia tamaa wamewaacha wenye mji wafanye watachojua wao with little interference