Vijana wa CCM onyesheni hasira zenu kwa mwenyekiti wenu kwa nini ateue waliofata teuzi na maslahi awaacheni nyinyi

Vijana wa CCM onyesheni hasira zenu kwa mwenyekiti wenu kwa nini ateue waliofata teuzi na maslahi awaacheni nyinyi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nyie vijana wa CCM, mimi nawaelewa kabisa hasira yenu.

Nyie mmepambana kukitetea chama, wakati hawa akina Lijualikali, Nassari, Mashinji wakipambana kuwatoa madarakani. Waliwaita majina yote yakiwemo "vijana wasiojielewa", "waimba mapambio", na majina kibao ya kejeli. Lakini leo hii wanahama vyama vyao kufuata masilahi na teuzi halafu nyinyi wakubwa wanawapita tu utadhani ni begi la misumari.

Nyie ndiyo mliohangaika kufanya kazi za chama, kunadi sera zake, na kufanya mipango ili chama kishinde, halafu fupa wanakuja kupewa akina Nassari, mtu ambaye kwanza alifukuzwa bungeni kwa utovu wa nidhamu.

Nyie vijana wa CCM, mnajua vizuri kuwa akina Nassari na Lijualikali hawakuja CCM kwa kuipenda CCM wala sera zake bali Walinunuliwa kwa ahadi za vyeo na fedha. Je mnakubali kuwa wao ni bora kuliko nyinyi?.

Mna haki ya kumchekea Mwenyekiti usoni ila mkigeuka kunjeni ndita

Mna haki ya kumshangilia Mwenyekiti mkutanoni ila mkitoka mzomeeni kimoyomoyo

Mna haki ya kumwambia Mwenyekiti asante, lakini kimoyomoyo mseme kuwa hapana.

Mna haki ya kumvisha kilemba cha ukoka Mwenyekiti wenu ila mkibaki peke yenu semeni kuwa amechemsha!

Mlichofanyiwa ni kuvuliwa nguo hadharani, waziwazi kuwa nyinyi ni mavuvuzela hamtoshi, bali wale wasaliti mamluki ambao hawajawahi kukifanyia chema chama ndo wanaonekana wa maana.

Vijana wa CCM poleni sana, Wakubwa wenu hawawaamini!
 
Vijana wa ccm siyo wajinga kama vijana wa chadema!

Kuna nafasi kibao ambazo rais Samia amewateua vijana wa ccm. Sasa hatuwezi kuharibu image ya chama chetu kisa chuki zenu kwa nafasi 3 za Lijuakali, Mashinji na Nasari.

Huu uteuzi wa awamu hii mama amewakomesha sana machadema sasa yanajribu ku divert ionekene vijana wa ccm ndio wanaumia.

Acheni ujinga jamani! Lowasa alipohamia chadema alipewa nafasi ya kugombea urais fasta fasta huku watu waliopigania chama kwa damu kama kina Slaa wakitukanwa na vijana watiifu kwa Mbowe! Same kwa Sumaye, Nyarandu na wengineo lakini sijawahi kuona vijna wa chadema wakionesha hasira kwa Mbowe!

Endeleeni kudemka! Si mlikuwa mnasema mama anawakomesha mataga? Mbona toka juzi mmechachama kama siafu kila bavicha anaanzisha uzi? Kuna nini huko bavicha na huu uteuzi?

Huu uzi wako una tofauti gani na ule wa bavicha mwenzio Mshana jr?

Na bado, tukiwambia ccm ni mfumo mnabaki mnakenua mimmeno hoo Samia siyo sawa na mwendazake! Sasa hivi vilio vyenu pelekeni ubelgiji.
 
Vijana wa ccm siyo wajinga kama vijana wa chadema!

Kuna nafasi kibao ambazo rais Samia amewateua vijana wa ccm. Sasa hatuwezi kuharibu image ya chama chetu kisa chuki zenu kwa nafasi 3 za Lijuakali, Mashinji na Nasari...
Vijana wa Chadema wanakuja huko kulamba teuzi kiulainiii, sasa ndo utajua nani mjinga, wale wanaolamba teuzi au wale wanaozunguuka na bendera ya jembe na nyundo huku wakipigwa chini
 
Watakuelewa kweli ? Wanatafunwa na unafiki wao maana walishangilia manunuzi wakayaita ni uungwaji mkono mkubwa wa chama chao kwa kazi kubwa kiliyoifanya sasa hawana uhalali wa kulalamika maana wakilalamika watadhihirisha yale madai ya manunuzi yalikuwa ya kweli 100%
 
Vijana wa Chadema wanakuja huko kulamba teuzi kiulainiii, sasa ndo utajua nani mjinga, wale wanaolamba teuzi au wale wanaozunguuka na bendera ya jembe na nyundo huku wakipigwa chini
Akili ndogo haiwezi kuona mbali!

Hao vijana si ndio mlikuwa mnawatukana kwamba wamenunuliwa na Magufuli?

Mkuu, kwanini unakuwa na akili ndogo namna hii?

Mashinji, Lijuakali na Nassari tukifikiri mmewasahau kumbe bado wanawauma sana?
 
Wewe na wenzio Igu mnateseka kweli kweli tena kwa kiwango cha lami.
 
Akili ndogo haiwezi kuona mbali!

Hao vijana si ndio mlikuwa mnawatukana kwamba wamenunuliwa na Magufuli?

Mkuu, kwanini unakuwa na akili ndogo namna hii?

Mashinji, Lijuakali na Nassari tukifikiri mmewasahau kumbe bado wanawauma sana?
Nyie pigeni makelele mitandaoni, huku vijana wa Chadema wakinunuliwa na kupewa mavyeo huko
 
Sasa iweje wengine mnatukana watu humu kwa hasira zisizojulikana chanzo chake.
hao ni mamruki toka chadema wanajifanya wana ccm siyo kweli sisi ccm halisi tumetulia wala hatuna neno endeleeni na chuki zenu huko na chadema yenu msituletee ujinga huku
 
Mi nilichokiona ni kwamba vijana wa CCM ni vilaza.sasa mama mlitaka afanye nini kama sio kuchukua watu kutoka sehemu nyingine.vijana wenyewe waliyopo CCM ni watoto wa viongozi ambao wanapenda tu starehe kuliko kazi.tena kawaonea tu aibu,ilitakiwa safu nzima iwe watu waliotoka kwenye vyama vya uinzani
 
Nyie vijana wa CCM, mimi nawaelewa kabisa hasira yenu.

Nyie mmepambana kukitetea chama, wakati hawa akina Lijualikali, Nassari, Mashinji wakipambana kuwatoa madarakani. Waliwaita majina yote yakiwemo "vijana wasiojielewa", "waimba mapambio", na majina kibao ya kejeli. Lakini leo hii wanahama vyama vyao kufuata masilahi na teuzi halafu nyinyi wakubwa wanawapita tu utadhani ni begi la misumari...
Acha uchonganishi, Rais ni kiongozi wa watanzania na siyo wa chama tu...Inapokuja kwenye nafasi ya urais lazima aonyeshe kuwa ni rais wa wote wenye vyama na wasio na vyama....Jadili umakini na uwezo wao siyo vyama vyao vya siasa
 
Sasa kijana kama Nassari aliyefukuzwa bungeni kwa kukimbia vikao huku akilipwa mshahara kodi ya wananchi unaona anafaa kuliko vijana walioko ndani ya CCM?
 
Vijana wa ccm siyo wajinga kama vijana wa chadema!

Kuna nafasi kibao ambazo rais Samia amewateua vijana wa ccm. Sasa hatuwezi kuharibu image ya chama chetu kisa chuki zenu kwa nafasi 3 za Lijuakali, Mashinji na Nasari...
Idugende njoo usikie huku kuna mtu anawasemea vijana wa CCM wenye hasira. Njoo umpe vidonge vyake mkuu.
 
hao ni mamruki toka chadema wanajifanya wana ccm siyo kweli sisi ccm halisi tumetulia wala hatuna neno endeleeni na chuki zenu huko na chadema yenu msituletee ujinga huku
Sema tu kuwa ni hasira za kukosa teuzi,wakaguewenzio utagundua.
 
Back
Top Bottom