Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Nyie vijana wa CCM, mimi nawaelewa kabisa hasira yenu.
Nyie mmepambana kukitetea chama, wakati hawa akina Lijualikali, Nassari, Mashinji wakipambana kuwatoa madarakani. Waliwaita majina yote yakiwemo "vijana wasiojielewa", "waimba mapambio", na majina kibao ya kejeli. Lakini leo hii wanahama vyama vyao kufuata masilahi na teuzi halafu nyinyi wakubwa wanawapita tu utadhani ni begi la misumari.
Nyie ndiyo mliohangaika kufanya kazi za chama, kunadi sera zake, na kufanya mipango ili chama kishinde, halafu fupa wanakuja kupewa akina Nassari, mtu ambaye kwanza alifukuzwa bungeni kwa utovu wa nidhamu.
Nyie vijana wa CCM, mnajua vizuri kuwa akina Nassari na Lijualikali hawakuja CCM kwa kuipenda CCM wala sera zake bali Walinunuliwa kwa ahadi za vyeo na fedha. Je mnakubali kuwa wao ni bora kuliko nyinyi?.
Mna haki ya kumchekea Mwenyekiti usoni ila mkigeuka kunjeni ndita
Mna haki ya kumshangilia Mwenyekiti mkutanoni ila mkitoka mzomeeni kimoyomoyo
Mna haki ya kumwambia Mwenyekiti asante, lakini kimoyomoyo mseme kuwa hapana.
Mna haki ya kumvisha kilemba cha ukoka Mwenyekiti wenu ila mkibaki peke yenu semeni kuwa amechemsha!
Mlichofanyiwa ni kuvuliwa nguo hadharani, waziwazi kuwa nyinyi ni mavuvuzela hamtoshi, bali wale wasaliti mamluki ambao hawajawahi kukifanyia chema chama ndo wanaonekana wa maana.
Vijana wa CCM poleni sana, Wakubwa wenu hawawaamini!