LGE2024 Vijana wa CCM wamshambulia Mjumbe wa Kamati Tendaji ya CHADEMA katika Kituo cha Uandikishaji

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Nahapa ndipo napata majibu kwanini wananchi hawajitokezi kujiandikisha nannina hakika hawatajitokeza pia kupiga kura kwa mwenendo huu
Kajiandikishe usiogope tofali wewe kama raia mwema unayeenda kujiandikisha

Tofali zina wenyewe zinazowahusu
Wwwe kama raia mwema hata u9ne tofali zimepangwa mbele ya meza ya mwandikishaji hazikuhusu ziko pale kutumika kujenga ofisi zoezi la kuandikisha likiisha
 
Uchu wa madaraka unawatoa utu kabisa kwanini vyama vya upinzani vimekubali kushiriki huu ujinga? Wangewaachia tu uchaguzi wao wapate hayo madaraka wanayotaka.
 
Kupigana hadharani ni jinai polisi anatakiwa kum arrest mtu anayefanya fujo/shambulio la kudhuru mwili pasipo hata arrest warrant.
Mbona mabondia huwa wanapigana hadharani na kudhuriana mbona huwa hawakamatwi na polisi
 
Hapo mtu kutishwa tofali la kisogo. Dah!

Sitokaa nisogelee vituo vya kura maisha!

Watu wamekuwa wa ajabu sana!
 
Kwaiyo hao kenge wa Kijani nao wote ni mawakala kwenye hicho kituo na wenyewe wapo eneo hilo kufanya nini kweli hujitambui wewe
 
Kwaiyo hao kenge wa Kijani nao wote ni mawakala kwenye hicho kituo na wenyewe wapo eneo hilo kufanya nini kweli hujitambui wewe
Heading ilitakiwa iseme wanaodhaniwa wana CCM

Moderators badilisheni heading.Hakuna ushahidi kuwa ni wana CCM waliomtandika tofali
 
Mbona mabondia huwa wanapigana hadharani na kudhuriana mbona huwa hawakamatwi na polisi
Ule ni mchezo rasmi unaotambuliwa na sheria hadi za kimataifa na una chama chao cha mabondia.

Mchezo wa bondia unasimamiwa na mwamuzi ambaye anazielewa sheria za mchezo husika vilivyo.

Sasa mkuu kama kitu kidogo kama hiki umeshindwa kutofautisha utaweza kufanya reasoning ya mambo yanayohitaji IQ kubwa?
 
Wakati huo usisahau anaye pigwa na tofali bila hatia ni binadamu mwenzako hata kama hujali na ni mtanzania na ana ndugu na wana jamii kama wewe, raia wanaona ndio maana hawana namna ya kujibu mapigo kwa sababu jeshi mnalo na mitutu mnayo wao wameona wakae kando tuu kwenye hili zoezi ndio maana hawaonekani vituoni kujiandikisha na hapo bado kupiga kura ndio kabisaa, mnaweza dhani njia za kujeruhi, kuumiza na kuua ina afya kwa ustawi wa chama na nchi kumbe ndiyo mambo yana haribika zaidi .

Mimi ni mwana CCM kamili nina kadi na nina ilipia, lakini sijawa mfuasi mjinga wa kuunga mkono hata mambo ya hovyo hovyo yanayo fanywa na wanachama wasio na weledi
 
Mbona wote ni cdm?
Watakuwa wanagombea nini, ama mshiko?
 
Kupitia hiyo klip utajua mwana-CCM ni yupi na Chadema ni yupi?
Kwa nini huyo alopigwa na tofali asiwe mwana-CCM?
Wakati mwingine tuwe tunabalance mambo.
 
Ndiyo tumefika hapa?🥹🥹🥹
 
Hivi Kuna mtu alikuwa na nguvu kama Adolf Hitre,lakini mwisho wake ulikuwaje
 
Ndiyo kazi ya ccm hiyo.
Ukisikia AMANI NA UTULIVU ndio hiyo ndugu, yaani mpinzani akifanywa hivyo ni sawa tu, wala askari hafanyi chochote na huyo jamaa badala ya kupelekwa kwenye vyombo vya dola utasikia kapewa cheo cha uDC. Hiyo ndio Tanzania ya chifu Hangaya.
 
Siasa ni uadui?
 
Ndio alitakiwa apigwe na tofali? Polisi wamechukua hatua gani?
 
Lakini ndrugo zangu wanachadema mambo mengine mnajitakia tu, huhusiki na zoezi la uandikishaji unahoji nini huenda vijana wanajiandikisha kwenda kucheza mechi ya kirafiki na wenzao eneo la mbali...

by the way who are you?
si majuzi hapa mlitangaza kuna kituo cha kupokea changanoto za zoezi la uandikishaji, sasa mchungaji si angerepoti huko?

Lakin mbona kama vile mtu kapigwa ngumi, upper cut chembe la kidevu, lazima ukae, unasema kapigwa na tofali? au ngumi ilikua ngumu na kali sana ?🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…