Angalia simba day ndo utaona maandalizi siyo ya wiki moja au mbili,zile pattern zilizochorwa pale uwanjani ndo utajua walikuwa na maandalizi ya kutosha na yanachukua muda. Na pia suala siyo miezi mitatu au minne suala ni lengo lake ni nini . Na usiyaite mafunzo hayo siyo mafunzo kwamba yana qualify kupewa cheti, ni event tu imeandaliwa basi ikiisha imeisha ikija event nyingine itahitaji set up nyingine. Sasa huwezi kuita shule nzima lazima kuchagua wachache sababu ile siyo haki ya kila mtu ni tukio tu limejitokeza unachukua watoto wachache basi wanafanya linaisha. Ni mambo ya kawaida sana kama unavyoona watoto wanatengeneza nyimbo na michezo Kwa ajiri ya kusherehesha kaka au dada zao kwenye graduation Kwa shule husika. Sasa watoto wakiandaa wimbo au mchezo kwa zaidi ya mwezi Kwa ajiri ya graduation tena Kwa kusimamiwa na walimu wao huwezi Sema wapewe vyeti. Ni mambo ya kawaida kabisa. Tulikuwa na michezo mashuleni na tulijiandaa kwa muda mrefu na kilikuwa kipindi pendwa kwa wanafunzi. Mechi tu ya shule na shule wanafunzi wanapiga zoezi miezi kadhaa sembuse hako katukio kadogo kwamba ndo wapewe cheti 😂😂. Sasa mtu si atamaliza chuo amejaza kabati la vyeti