Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Kwa tathmini yangu, kama kuna kundi ambalo future yao imeharibiwa sana na sera, maamuzi na mienendo ya serikali ya Magufuli, basi kundi hilo ni la vijana.
Kwanza, tukianzia kwenye sheria kandamizi zinazotingwa kila siku ambazo zinafunga mianya hata ile midogo iliyokuwa imebaki ya vijana kuweza kutoboa. Sheria za mitandao kwa mfano.
Tukija kwenye maamuzi ya kiuchumi na kifedha. Pesa nyingi iliyotapanywa kinyume cha sheria na serikali katika kufanya manunuzi yasiyo na tija ingeweza kutumika kuboresha elimu na mazingira ya vijana kuweza kutoboa kimaisha.
Tatu, maamuzi ya kuminya uhuru wa kuongea una athari zaidi kwa vijana. Kina Mdude, Tito, Kabendera, Saanane wanawakilisha alama ya vijana victims wa serikali hii.
Ujana ndiyo kipindi mtu anakuwa huru zaidi, spirit yake inataka kujaribu vitu tofauti, inajenga uwezo wa kuangalia mambo kwa mitazamo mipya na kukosoa. Ni miaka ya kuwa rebellious. Ndiyo miaka tunawakosoa hadi wazazi wetu. Ni natural process katika makuzi ya binadamu. Magufuli na serikali imenyima fursa hiyo kwa kizazi hiki cha sasa na itaenda kuwaathiri katika maisha yao yote.
Tundu Lissu, baada ya masaibu yake, angeweza kutulia zake huko Ulaya akala maisha yake fresh tu. Wengi tusingemlaumu.
Ila kwa mapenzi yake ya dhati kwa taifa hili, ameamua kurudi kuwapambania nyie vijana na future yenu. Tafadhali msimuangushe. Mnahitaji kuongeza juhudi kusimama naye na muwe mstari wa mbele kulinda kura na kupinga mbinu zozote zile za kuharibu zoezi la kura. Future yenu inategemea sana matokeo ya uchaguzi huu.
Mwisho nawahusia vijana, chagueni Tundu muweze kutoboa!