Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Vijana hao wenye ujuzi katika uhandisi wa kompyuta, IT na mawasiliano ya simu waliambatana na Mhadhiri msaidizi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Mhandisi Jumanne Ally ambapo wanafunzi zaidi ya 470 kutoka nchi 49 duniani walishiriki mashindano hayo.
Waziri Nape amesema kuwa ushindi huu unaonyesha uwezo uliopo miongoni mwa vijana wetu wa kitanzania katika fani muhimu za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Vijana hao watarudi Tanzania tarehe 28 Mei, 2024 na wanawatarajiwa kupokelewa kwa shangwe na kupongezwa kwa kuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine wa kitanzania.
Waziri Nape ameuzungumzia ushindi huo kuwa mwanzo mzuri wa kujenga taifa lenye ubunifu katika fani za TEHAMA.