Vijana wa Kiume badilikeni

Vijana wa Kiume badilikeni

Mrs Gudman

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2015
Posts
613
Reaction score
1,297
Habari za jumapili wana Jamii Forum

Leo naomba nizungumze kidogo na hawa wenzetu upande wa Kiume mana miaka ijayo kuna hatari ya kupoteza nguvu kazi

Siku izi ni kawaida kabisa kukuta mdada anauza matunda, anatembeza mtumba, anachoma mandazi ubuyu na juice na mengine mengi ya kuingiza kipato, huko kwenye vikoba ndo usiseme wanawake wameamua kutafuta hasa tofauti na zamani

Lakini upande wa pili kuna uvivu na kujisahau ambapo trend ikiendelea hivi kuna hatari kubwa mbeleni
Wanaume hasa hawa wanaojiita graduate mnapotea kaka zangu, najua mmesoma bodaboda mnaona si hadhi zenu tena, saidia fundi pia siyo hadhi yenu kuuza matunda siyo hadhi yenu mmebaki mnatembea na bahasha kutwa kutafuta kazi, ebu ndugu zangu acheni u brazamen wa kishamba, jichanganyeni hakuna pesa inakuja kukugongea mlango lazima tu uitolee jasho kidogo, mbona wadada wazuri tu wanajishughulisha??

Kuna mtoto wa ndugu yangu alifikia kwangu ili aende interview jamani anaamka saa tano akiamka anaamka na laptop na muvi, anakunywa chai anaendelea na muvi mchana anakula anaendelea na muvi narudi nyumbani nipo hoi bin taaban yeye hata kuoga ajaoga,saa mbili na nusu tunakula dinner ndo anamwambia dada akampashie maji ya kuoga [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivi huyu mtu hata akipata kazi si mzigo huu??????

Huu ni mfano lakini wanaume wa aina hii ni wengi sana

Wakati ambapo dunia ipo busy kuimpower mtoto wa kike hebu Wazazi wekeni juhudi kidogo na kwa watoto wa kiume, wajitambue na kuwafundisha kufanya kazi kwa mikono yao wenyewe.

Ni aibu sana

1619958405280.png
 
Kiukweli mimi sijui tunakoelekea.

Na sasa hivi naona wanawake wanatafuta pesa wakipata, wao ndio wanaoa.

Shilole kila siku yeye ndio anaoa.

Wanaume wamegeuka wengine mashoga, wengine chawa, wengine omba omba wa kutisha aisee.

Sijui miaka 10 mbele itakuwaje.

Taasisi ya Familia imetikisika.
 
Kiukweli mimi sijui tunakoelekea.

Na sasa hivi naona wanawake wanatafuta pesa wakipata, wao ndio wanaoa...
Ni kweli kaka

Ile women empowerment imeleta matokeo chanja sana, kiukweli wanawake wanaobweteka wamebaki wachache nao hao wachache utakuta kuna sababu inayomkwamisha tu

Lakini mwanamke ukimuonyesha njia anafanya wonders, leo wanawake wanacheza vikoba, sijui upatu, kuuza vitenge karanga etc ila wanaume sijui wamepatwa na nini kabisa yani wamebaki kubeti kamari bangi na vitu vingine vibovu tu

Kuna mahali tulikuwa na kikoba watu kumi among of us 9 ni wadada na mmoja ni mkaka, uwezi amini yule kaka tulijuta kumuweka hana plan yeyote, tunakutana kila tarehe mbili ya mwezi unaleta hisa na kama una rejesho unapeleka, yule kaka siku inafika haji wala aleti pesa, siku akija awe alikuwa ana shida ya hela wala hana akisikia tu kuna hela anataka kukopa hata kama hana shida imagine anakopa anaenda kutowa watu out au basi anaenda kula tu basi tukaona huyu anatupotezea muda tukamtowA
 
Ni kweli kaka

Ile women empowerment imeleta matokeo chanja sana, kiukweli wanawake wanaobweteka wamebaki wachache nao hao wachache utakuta kuna sababu inayomkwamisha tu...
Binafsi naona tatizo limeanzia kwa wazee wetu ambao ndio walezi. Ni kama wamekata tamaa.

Walimu pia wamebadilika siyo kama waliotufundisha, kila mmoja ana mambo yake siku hizi.

Sasa hivi watoto wanalelewa na walimwengu, TV na mitandaoni.
 
Binafsi naona tatizo limeanzia kwa wazee wetu ambao ndio walezi. Ni kama wamekata tamaa.

Walimu pia wamebadilika siyo kama waliotufundisha, kila mmoja ana mambo yake siku hizi.

Sasa hivi watoto wanalelewa na walimwengu, TV na mitandaoni.
Aiseee
 
Binafsi naona tatizo limeanzia kwa wazee wetu ambao ndio walezi. Ni kama wamekata tamaa.

Walimu pia wamebadilika siyo kama waliotufundisha, kila mmoja ana mambo yake siku hizi.

Sasa hivi watoto wanalelewa na walimwengu, TV na mitandaoni.
Ni aibu sana kwakweli.

Huku uswahilini unakuta kwenye vibanda vya cd kuna vijana wadogo wamejazana hadi usiku wamenyoa viduku huku wakijifanya kina diamond,

Unajiuliza huyu kabisa muda huu ndio anarudi kwangu ananikuta mimi ndio babake anagonga anaingia kulala.. Hiiiiiiiii
 
Katika siku ulioongea point ni leo mtu yan hana alternative ya kutafuta hela mzee mwenzangu me hawa watoto wakiniomba msaada sikuiz huwa nawapa jero wakabeti labda atabahatisha sababu akienda akikosa mara kumi ndio atajua hela kuipata sio rahis kama wanavyodhani. Watu kama hao wapo wengi tumekutana nao kwene ma interview utawaonea huruma yan kujieleza hawez kabisa sasa sijui tatizo huwa nini daaah
 
Habari za jumapili wana Jamii Forum

Leo naomba nizungumze kidogo na hawa wenzetu upande wa Kiume mana miaka ijayo kuna hatari ya kupoteza nguvu kazi...
Tatizo kubwa lipo kwenye jamii sio vijana.. yani kijana akimaliza chuo akaendesha bodaboda au kufanya Kazi ya saidia fundi watu wengi huanza kusema vibaya kumchukulia kama kitendo cha kwenda shule alipoteza muda.. na hakuna maarifa aliyo yapata ya ziada tofauti na walio baki mtaani hii kitu sio kizuri kwenye jamii yetu, na ndo kimefanya vijana wengi wajifungie majumbani.

Yani ili nchi iendelee inatakiwa tujifunze kuwasifia watu wanao kujituma kufanya Kazi kwa bidii hata kama ikiwa ni Kazi ya kuzibua choo.. na kingine pia tujifunze kwa nchi zilizo endelea.

Jamii yetu inaona kama mtu ukimaliza kusomea Uhandisi ukaenda kulima au kujiajiri katika fani tofauti unakuwa umepotea.. kwa mtazamo wangu kitu kikubwa kinacho kwamisha vijana ni majungu kutoka kwenye jamii.

Mfano niulize tu.. ni wazazi wangapi wataruhu mwanao aliesomeshwa kwa gharama mpaka chuo akawe bodaboda,saidia fundi, au hata kuwa mpishi mgahawani?? Wazazi kama mpo humu naomba mjibu kwa uwazi kabisa [emoji1488]
 
Back
Top Bottom