Vijana wa Kiume badilikeni

Kingine wanawake wanapendana wananyanyuana wanapeana connection masela 80% hatupendani.....
 
Wanalinda brand.

Pisikali itanionaje nabebeshwa mizigo wakati inajua, mimi ni Uni Graduate laptop na movie kila time
 
Wanalinda brand.

Pisikali itanionaje nabebeshwa mizigo wakati inajua, mimi ni Uni Graduate laptop na movie kila time
pisi kali kama huna mpunga wanakuona mwenzao tuu...
 
Usiongee ili kufurahisha genge wapi unapata kazi ya ulinzi siku hiyo hiyo?
Binafsi nilivyomaliza chuo baada ya kudhurula na bahasha ikabidi niingie kitaa kutafuta kazi uko mtaani hakuna kazi kama mnavyosema labda kazi ya kuuza karanga,nimehangaika ktk kampuni kibao za ulinzi sijapata kazi zaidi ya kuambiwa toa elfu 80 tukupe kazi,hata saidia fundi bila connection hupati.
Ila mwisho wa siku nikaja kutusua kizali la mentali
 
pisi kali kama huna mpunga wanakuona mwenzao tuu...
Inapigwa sound tu na mipango kama yote.

Pamba zimenyooshwa, chini laba kali au four ange imepigwa kiwi halafu imewekwa juani. Machoni glasses.

Bahasha kubwa la kaki, mkononi saa na iPhone ( hata kama ya Laki used ulinunulia boom ).

Stori kama zote, kwamba kuna maboss kibao wanataka ukapige kazi, ila mshahara wa 1M haukutoshi yaani🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu uko wapi na ulienda kampuni zipi??

Usiongee usichokijua
 
Mkuu naomba mniunge na mm huko vikoba
 
Polen sana kwetyu huku vijana tunashindana kununua ma v8,
 
Mkuu uko wapi na ulienda kampuni zipi??

Usiongee usichokijua
Kwanini unasema nisiongee nisichokijua wakati mimi ndio niliyekuwa natafuta kazi na nimejionea.
Kampuni ni hizi
G4S, rampart,kk,chui,guard, giant security ,maridadi nk nyingi
Msifikirie uku mtaani kazi ni rahisi,kama wewe ulibahatika shukuru Mungu
 
na vikipewa mzigo kibao kimoja....kinawahi home wasifunge gate......
 
Wengi Wanapenda sana kulaumu, ujuaji na ubishi.
Kuna baba mmoja alikuwa anasema vijana wengi siku hizi hawajitambui.
Wengi wao wapo hapa JF, kucha kutwa kumnang'a Marehemu. Na wengi kama Erythrocyte wanahangaika kusambaza hoja za kitoto hapa JF baadala ya kufanya kazi. Hawajui huyo ni binti na anaoleka! Retired, Mshana Jr, brazaj Quinine BAK jitambueni, achana na masuala ya kusifia Chadema, piga kazi
 
Kwanini unasema nisiongee nisichokijua wakati mimi ndio niliyekuwa natafuta kazi na nimejionea.
Kampuni ni hizi
G4S, rampart,kk,chui,guard, giant security ,maridadi nk nyingi
Msifikirie uku mtaani kazi ni rahisi,kama wewe ulibahatika shukuru Mungu
Mkuu labda nikupe mifano:

Gardaworld hawapokei rushwa hata 100 ila masharti yake tu yatakukimbiza kama huna.

Nenda G1 security hakuna rushwa kabisa, tena wao wanataja tu cheti cha kuzaliwa hata kama Drs 7.

Nenda Simplisafe siku hiyo hiyo unapata kazi.

G4S ndio huwa rushwa fulani hasa wakati wa stage za mitihani.
 
Mada ni nzuri sana.Hili ni janga la Taifa.

Vijana wa siku hizi ni majanga sijui hata walezi/wazazi wanakosea wapi kwa kweli?Siku hizi kwa kijana kutokuwa na kazi ni jambo la kawaida sana hata wanachukulia poa kutafuta wanawake walowazidi umri ili wahudumiwe kwasababu wanakwepa majukumu kama wanaume.

Watu wengi walofanikiwa kutoka kimaisha wameanza chini yaani katika maisha haya usitegemee kila kitu kitakuwa served in a silver platter.Inabidi vijana wajifunze kuchakarika kwa kweli na kutafuta njia nyingine za kipato kama njia mmoja haifanyi kazi.Lazima mtu siku zote Uwe na plan B kama plan A haifanyi kazi.

Kuna watu wana elimu zao na master degree na wanalima bamia vilevile kama njia nyingine ya kuingiza/kuongeza kipato.Kwangu mimi huyo ni mtu anayejituma hasa kuliko mtu anayekaa akizembea.

Kuuza karanga au kahawa mbona ni kitu ambacho walichokuwa wanakifanya wanaume mainly approximately 15 yrs ago.Kwanini sasa Kwa wakati huu iwe kituko?Kazi ni kazi bwana hakuna kuchagua kazi,mwanaume ambaye anaona bora akae alishwe na kuhudumiwa na wengine kuliko kufanya kazi ya chini si mwanaume. Mwanaume hapaswi kuchagua kazi. Muhimu mkono uende mdomoni na chakula kiwepo mezani.

Vijana wakiume inabidi waache kulemaa na kuzembea na waanze kujituma haswa.
 
Baadhi ya wazazi wanaona hata ni mkosi na wako radhi kuzungusha watoto wao kwa waganga wasafishwe nyota
 
Hali mbaya sana kila mtu amekaa kwenye mgongo waukosefu waajira halafu watoto wakiume ndoinaonekana wanakosa sana ajira
Mtoto wa kiume hana fursa za kuaminiwa haraka na pia jamii iliwaaminisha baadhi ya Kazi kama za mgahawa,kuuza mboga,kuchoma chapati au kuuza juice fresh au mkaa wa kupanga kwamba ni Kazi za wanawake ndio maana unaona hivyo.
 
Kwaiyo Shemeji umeona uje uni chomee uku na picha yangu ume weka
 
mkuuu nenda kwa mama ntilie kaoshe vyombo uone utapewa shingapi per hour nina bro wangu alikua anipiga shule nchi za wenzetu kwenye mgahawa ila per hour alikua anachukua dau nono tu kiasi cha kuni uspport ada ya chuo
 
Mkuu, samahani, kumbe wewe ni KE?!

Umekosa picha ya KE hadi unaweka picha ya ME mbabu kwenye avatar yako?
 
Mengi yanaweza kuzungumzwa hapa lakini nafikiri mtu ukiwa nauhakika kidogo ndohapo utamsikia ajira sijapata hata ss wengine tukomtaani tunapigika na baadhi yawatu wanaweza kutuweka kwenye mifano kwawengine lakini ukweli nikwamba kinachotuongezea mwendo sio kwamba tunabidii sana aumaarifa sana nyuma yetu hakuna wakumtizama akupe chochote kama huna changamoto ubongo unalala
 
Mtu ana comment hapa anasema hapa Dar huwezi kosa kazi ya laki mwezi afu hasemi wapi....!!

Mwingine sijui ulinzi sawa ulinzi kazi zipo toa code kizazi kampuni gani watu wafike wakajaribu bahati zao..

Sio lawama tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…