Kwanza kabsa huyu anaejiita handsome ni fala na shoga wa dar.
Mimi nusu ni mtu wa chuga nusu mbeya,nimekaa mbeya almost 20 years.ngoja nikupe sifa za watu wambeya
Kwanza ujue wenyeji wambeya mjini ni wasafwa sio wanyakyusa,ila wanyakyusa wametawala hadi mbeya mjini kutokea pande zote za mbeya haswa kyela na tukuyu.
Mbeya ni mchanganyiko wamakabila mengi na moja ya makabila wenyeji,ni wandali,wamalila.... Na hapa pana wakinga ,wachaga nk
Sifa kuu ya mbeya ukizaliwa hapa hata uwe kabila gani lazima utakua na mbeya blood ndani yako.
Watu wa mbeya ni veeeery proud wa mji wao sijawahi ona popote yani.na ujue izo b na sugu si wanyakyusa kama unavyodhani.
Alieseme watu wambeya ni enfirior au waoga sijui is totally wrong.watu wambeya wengi wanaconfidence na over confidence kupitiliza.wapo wapole ndio lakini wengi wao ni waongeaji .
Si wachokozi ila ni washari sana na usiombe umchokoze MTU wambeya unaweza juta na popote walipo wanajua kujichanganya sana na wanaushirikiano mno na kila walipo wanataka wajulikane wametoka mbeya.nimezunguka mikoa mingi tz karibu yote nimeona wapo na jezi zao za mbeya city mgongoni na wanajivunia sana kwao
Huwez kumshinda ujanja mtoto wambeya aisee asikudanganye MTU.labda awe boya tu mwenyewe.
Ukitaka kujua kichaa cha wanambeya nenda mbeya siku mbeya city inacheza na team yoyote alafu wafungwe au washinde uone moto.kuna wadada wamedata hakuna mfano.
Watu wambeya ni veeery smart mifano IPO mingi kupitiliza na wanapenda sana kuvaa mana chakula si tatizo.
Unapozungumizia masuala ya wanyakyusa wakyela na tukuyu hayo yapo hivi.
Wanyakyusa wakyela ni wakarimu,wasafi kupitiliza,suala ni kwamba wanyakyusa wengi ni waongeaji ila wakyela ni kama wazaramo na hii inatokana na mazingira yao,kyela ni kama pwani aliefika pale anajua.wapo too proud of themselves na ofcoz wanajeuri lakini si ya kumdhuru MTU.
Watukuyu hawatofautiani sana na wakyela kama jeuri wanyakyusa wote wanayo ila ni wakarimu sanaaa.
Hakuna mji umekaa vizuri kama mbeya ,mbeya huwezi kufa njaa.
Alosema mbeya wanaiga chuga uhiphop ngoja nikusahihishe,mbeya INA nature ya uhiphop kitambo unaweza fatilia history hata ya wasanii wengi walosoma na kukaa hapa.baridi flan LA mbeya na life style ya kigansta inafanya mbeya iwe kama chuga na ndiomana wambeya wengi hupenda chuga na chuga wanapapenda mbeya.
Mbeya huwezi survive bila akili sababu vyakula vingi mno lakini haso ya kuishika pesa usiombe yaani.
Kuna mzuuuri mengi sana kuhusu mbeya
Sent using
Jamii Forums mobile app