On Duty
JF-Expert Member
- Aug 21, 2020
- 566
- 1,083
Wasaalam ndugu zanguni,
Katika tafiti zangu ambazo nimekuwa nikizitafiti takribani miaka
isiyopungua kumi(10). Nimekuja kugundua kwamba hawa vijana wa hapa DSM ni mzigo usio wa kawaida.
Ukipita mitaa ya Mwananyamala, kigamboni, kimara, makumbusho , kinondoni yaani hawa vijana sijui wapo katika sayari ipi! Lugha yao kuu ni matusi.
Yaani hawa watu ni wavivu zaidi ya uvivu sijui hata tuwaweke kundi gani kwa maana hawana kazi lakini hawapendi kazi. Kutwa nzima wanashinda vijiweni wenyewe wanaita maskani wakigongea vimiamia vya wapita njia. Yaan mtu anatoka mihangaiko yake halafu wao wanafosi wapewe hela yaan bila aibu utasikia mjomba fosi hata jero basi tuongezee tukachukue kiki...what a pit!
Halafu ukiwaambia kuwa huna wanakutolea vitisho na wataanza kukuwinda usiku yaani watakutambua kama adui yao (unawapinga).Siyo kama wana uwezo wa kukupiga La hasha, ila hiyo mivagi ndiyo inawavimbisha vichwa maana hata ukikutana nao unawaonea huruma jinsi walivyochoka. Lakini ukiingia kwenye anga zao na kuwanyenyekea sana ujue watakupiga bisibisi maana ndo wanachoringia halafu ni wana umoja usio wa kawaida.
Ukiachana na hayo yote kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba wengi wao wazazi wao wanahangaika kutafuta chochote ilimradi mkono uende kinywani wao wanadhurura tu. Mama zao ni mama ntilie wa mtaji usiozidi elfu kumi na tano yaani wanakaanga mihogo, maandazi, na miguu ya kuku, na wengine wanauza uji asubuhi na jioni lakini wanawalisha vijana wao wenye miaka kuanzia 22-37 wakiwa na nguvu zao za kuweza kujitegemea.
Vijana wa DSM badilikeni na msiwe vilaza kiasi hicho et katoto ka pre-form one kanavuta ngada aisee. Jamani mkiombwa pesa na hawa wapumbavu msiwape maana mnawalemaza akili na kuwafanya washindwe kujitafutia na kusaidia wazazi wao.
Mimi ukiingia kwenye anga zangu, nakumwaga kifusi dadeq. Siwezi nikakupa hela yangu ukalewe ili upate nguvu ya kukaba watu hapo najua mama zenu kipaumbele kuwatetea kwa ujinga.
Omba samaki upewe nyoka!