Nimewasililiza wapinzani Lema na Lissu leo wakiongea kwenye youtube. Wameongea sio kupinga ya CCM bali kueleza hali ya vijana wetu Tanzania.
Wanasema wamechoshwa na watu ambao wana tuma private message eti wenyewe ndiyo wawaseme wengine wakiwa wameonewa kazini, wengine wakiwa wame pewa kesi za uongo na hata wengine kuwa wanaomba waongelee tozo.
Sasa vijana wa Tanzania ni lazima mjue hamuwezi kutegemea Lissu ambaye amepigwa risasi za miguu ndiye arudi na kuandamana kwasababu yenu wakati vijana wenyewe hamjali na ni waoga wa kusema vitu. Katiba mpya haitamsaidia Lissu zaidi ya nyie wenyewe.
Lissu ana elimu ambayo inamwezesha kupata kazi yeyote kuanzia professorship, UN, IMF na hata biashara kama speaker kwenye kampuni tofauti. Lakini hawa watu wengi kwenye siasa ni wasomi na wanaweza kufanya mengine mengi. Ili mueeze kuwa na future nzuri ni lazima muwe mstari wa mbele kufanya yafuatayo
1. Vijana bila kuvunja sheria pigania katiba mpya.
2. Katiba mpya unauopigania hakikisheni inaundwa na wataalamu kama Kenya na sio mabunge ya kisiasa.
3. Piganieni uhuru wa vyombo vizuri vya habari. Sio vile vya kili kila siku.
4. Pendeni watu wa makundi mengine sio wanasiasa na wasanii pekee. Yaani pendeni sana wafanyabiashara wazalendo na jifunzeni kwao.
5.Msiogope kuwa tofauti na watu wengine. Ubunifu ni muhimu.
6. Pendeni kusoma vitu na kuwa wafuatiliaji mfano inakuwaje sasa ndiyo mnajua kuhusu tozo wakati zilikuwa zinajadiliwa sana bungeni?. Ni wakati wa kuamka na kujua kila kitu kinakuhusu. Hivi unafikiri Lissu tozo zina muumiza kuliko wewe? Sasa kwanini una msubiri Lissu. Na nasema hivi nikiwa naunga mkono tozo.
7. Jielimishemi hasa kwa kuuliza maswali wakubwa wenu. Hata hapa tumia watu kujifunza na sio kubishana kila wakati na kupiga madongo.
8. Fikiria mbele sio leo au kesho.
9. Usiogope kuhama na kubadilisha mazingira.
10. Mwamini Mungu na sio makanisa au misikiti. Weka uhusiano wa moja kwa moja na Mungu. Mpe pesa mtu anayehitaji kama mgojwa, mtoto wa shule kabla ya masadaka ambayo yanaliwa.